Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuko pamoja na serikali ya Sudan Kusini katika vita dhidi ya COVID-19:UN

Tuko pamoja na serikali ya Sudan Kusini katika vita dhidi ya COVID-19:UN

Pakua

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umetangaza hatua mpya katika kusaidia juhudi zinazoongozwa na serikali ya Sudan kusini katika kuzuia na kujiandaa na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19. Grace Kaneiy ana ripoti kamili.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hii leo nchini humo imesema hatua hizo zinalenga kuwalinda watu wa Sudan Kusini na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Hivi sasa hakuna kisa chochote kilichothibitishwa cha COVID-19 nchini Sudan Kusini na operesheni za Umoja wa Mataifa zinaendelea kama kawaida kwa sasa nchi nzima za kutoa ulinzi, misaada ya kibinadamu na kusaidia shughuli za maendeleo.

Taarifa hiyo ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , UNMISS na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yanaheshimu na yatafuata maamuzi yatakayofanywa na serikali ya Sudan Kusini kulinda umma dhidi ya COVID-19 ikiwemo vikwazo kwa wasafiri kuingia nchini humo.

Na matokeo ya hatua hizo , wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walioko likizo hivi sasa wanashauriwa kutorejea isipokuwa tu wale wanaelezwa kuwa ni wa lazima kwa ajili ya operesheni za Umoja wa Mataifa . Na kwa mantki hiyo wafanyakazi watatakiwa kujitenga kwa siku 14.

Umoja wa Mataifa Sudan kusini pia umeamua kusitisha safari zote za wafanyakazi za mpango wa mapumziko ujulikanao kama R and R hadi tarehe 15 Aprili ambapo hali itatathiminiwa tena.

Pia shughuli na matukio yote ambayo yatahusisha idadi kubwa ya watu zimesitishwa kwa kuzingatia ushauri wa serikali kuhusu kulinda afya ya umma.

Suala linguine ambalo limesitishwa kwa mud ani hatua ya kubadilisha walinda amani na umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba utaendelea kusaidia juhudi za serikali katika kuzuia na kujiandaa kukabiliana na COVID-19.

Audio Credit
UN News/ Grace Kaneiya
Sauti
1'46"
Photo Credit
UNMISS/Isaac Billy