Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 MACHI 2020

19 MACHI 2020

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Licha ya kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa COVID-19 serikali ya Uganda imefunga shule zote hadi vyuo vikuu katika maandalizi ya kupambana na mlipuko endapo utazuka ugonjwa huo

-Nchini Sudan Kuisni Umoja wa Mataifa umechukua hatua madhubuti kuisaidia serikali maandalizi ya vita dhidi ya COVID-19 kwa umma na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kupitia hatua kadhaa

-Nako nchini Tanzania wafanyabiashara ndogondogo waelezea mlipuko huu wa COVID-19 unamaanisha nini kwao na athari zake wakati nchi hiyo ikitangaza idadi ya wagonjwa kufikia 6.

-Makala yetu leo inatupeleka wilayani Pangani Tanga Tanzania kusikia maoni ya wananchi kuhusu COVID-19

-Na mashinani leo utasikia ujumbe wa shirika la afya duniani WHO ulifafanua je uvae barakoa ya kitabibu  katika kujikinga na COVID-19 na uvae vipi.

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration
12'32"