Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania visa vya COVIDI-19 vyaongezeka, wafanyabiashara wateta

Tanzania visa vya COVIDI-19 vyaongezeka, wafanyabiashara wateta

Pakua

Nchini Tanzania  maambukizi ya virusi vya Corona au COVID-19 yameendelea ambapo hii leo wagonjwa wapya wawili wote wakazi wa Dar es salaam wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo baaada ya mmoja kuingia nchini kutoka safari ya Denmark, Uswisi na Ufaransa huku mwingine akiwa amerejea kutoka Afrika Kusini. Wagonjwa wote hao sasa wako chini ya uangalizi.

Hayo yakiendelea baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo wamezungumzia kile ambacho wanakumbana nacho huku wakisihi wananchi wazingatie hatua za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo. Stella Vuzo wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam na taarifa zaidi.

Eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam nchini Tanzania, wananchi wakiwa katika harakati za manunuzi wakati huu ambapo tayari taifa hili la Afrika Mashariki limethibitisha kuwa na wagonjwa wa virusi vya Corona.

Manunuzi yanafanyika huku baadhi wakiwa na barakoa kujikinga na Corona.

Katika viunga vya Namanga nako wilayani Kinondoni shughuli za zinaendelea za biashara na usafirishaji na kando tunakutana pia na mama lishe Binti Hassan ambaye yeye anazungumzia changamoto yao.

(Sauti ya Binti Hassan)

 Hata hivyo Binti Hassan anasema..

(Sauti ya Binti Hassan)

 Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO, hadi Jumatano kulikuwepo na wagonjwa 193, 475 waliothibitishwa katika nchi 164 duniani kote, na kati yao hao 7864 wamefariki dunia.

Audio Credit
UN News/Stella Vuzo
Audio Duration
2'7"
Photo Credit
UN News/ Stella Vuzo