Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

WFP yalalama kuporomoka kwa misaada ya chakula duniani

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limewasilisha ripoti mpya yenye mada isemayo: "Mtiririko wa Misaada ya Chakula Kimataifa", ambayo inatathminia huduma za ugawaji wa chakula ulimwenguni. Ripoti ilibainisha posho la chakula linalogaiwa umma wa kimataifa liliteremka sana katika 2007, kwa kiwango cha asilimia 15. Kiwanago hiki ni cha chini kabisa kushuhudiwa kimataifa tangu mwaka 1961.

KM atafanya mapitio ya ripoti ya tume juu ya usalama wa watumishi wa UM

Tume Huru Kuhusu Ulinzi na Usalama wa Watumishi na Majengo ya UM Duniani, iliobuniwa tarehe 05 Februari 2008, imemkabidhi KM ripoti ya uchunguzi ambayo ilipendekeza hatua kadha zichukuliwe kuimarisha usalama wa wafanyakazi wa UM, na pia kudhibiti bora hifadhi ya ofisi zake zilizotawanyika katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa katika mazingira ya ulimwengu uliofurika vitisho darmadaru aina kwa aina.

Mkutano wa UM kukabiliana na UKIMWI wakaribia kumaliza mijadala

Mkutano wa Hadhi ya Juu wa UM Kukabiliana na UKIMWI unatarajiwa kukamilisha mijadala yake baadaye Ijumatano. Ijumanne KM Ban Ki-moon alifungua Mkutano kwenye ukumbi wa Baraza Kuu, na alidhihirisha kwenye risala yake kupatikana mafanikio ya kutia moyo hivi karibuni dhidi ya janga la UKIMWI, na alitoa mfano wa maendeleo kwenye juhudi za kuawapatia wanawake na watoto huduma za afya kinga.

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda kukana makosa

Dominuque Ntawukuriryayo, aliyekuwa ofisa wa Serikali Rwanda na aliyetuhumiwa na Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) kuwa miongoni mwa wachochezi wa mauaji ya halaiki ya raia 25,000 wenye asili ya KiTutsi katika 1994, ameripotiwa kukana makosa mbele ya ICTR mjini Arusha, Tanzania.

ILO inapendekeza 'utandawazi unaohishimu haki za jamii'

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) ametoa mwito uitakayo jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura katika kukabiliana na athari haribifu zinazoletwa na "msawazisho wa shughuli za uchumi katika soko la kimataifa uliokosa haki za kijamii". Alitoa pendekezo hilo wiki hii kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 97 wa ILO mjini Geneva.

Mradi wa Milenia, Mbola watathminiwa na Mtafiti Mwandamizi

Katika makala zilizopita tulijadilia juhudi za za kuondosha umasikini za wanakijiji wa Mbola, na pia kuelezea ushirikiano walionao na wataalamu wa kitaifa, na kimataifa, kwa makusudio ya kuwasilisha mafanikio ya muda mrefu kwenye eneo lao, mafanikio ambayo yatafaidisha umma, kijumla.~~

Makundi yanayohasimiana Usomali kuridhia mwafaka wa amani

Makundi yanayohusika na mgogoro wa Usomali Ijumatatu yalibadili nia na kuamua kutia sahihi maafikiano ya amani kwa lengo la kukomesha uhasama kati yao. Maafikiano haya yalitiwa sahihi nchini Djibouti baina ya wajumbe wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho la Usomali (TFG) pamoja na wawakilishi wa upinzani wa Jumuiya ya Ukombozi wa Pili wa Usomali.

OCHA imeripoti mamilioni wanahitajia misaada ya kiutu Usomali

Katika mkutano na waandishi habari mjini Geneva, Elizabeth Byrs, Msemaji wa Shirika la UM juu Huduma za Dharura (OCHA), aliripoti kwamba mamilioni ya raia katika Usomali watahitajia kufadhiliwa, haraka, misaada ya kiutu ili kunusuru maisha ya umma ulioathiriwa na vurugu lilioselelea kwa muda mrefu katika taifa hili la Pembe ya Afrika.~~

Mtaalamu wa UM anakhofia athari za sheria mpya dhidi ya ugaidi Uingereza

Martin Scheinin, Mkariri Maalumu anayehusika na utekelezaji wa haki za binadamu kwenye mazingira ya ugaidi, ametoa taarifa maalumu, hii leo, yenye kuonya kwamba pindi Bunge la Uingereza litaamua mnamo Juni 11 kupitisha Mswada wa Kupiga Vita Ugaidi, anakhofia uamuzi huo utaathiri zile juhudi za kutekeleza haki za kimsingi, kimataifa, ikimaanisha nchi nyengine nazo pia zitataka kuigiza, na kuhalalisha sheria hiyo kwenye vyombo vyao vya sheria.