Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Vikwazo maalumu vyaongezewa muda dhidi ya Cote d'Ivoire

Baraza la Usalama limepitisha kwa kauli moja azimio la kuongeza, kwa mwaka mmoja zaidi, vikwazo vya biashara ya almasi na silaha dhidi ya Cote d’Ivoire. Vile vile azimio limepiga marufuku, na kuwanyima fursa ya kusafiri, baadhi ya raia wazalendo wa Cote d’Ivoire. Baraza lilisitiza ulazima wa makundi yote nchini kuwaruhusu wajumbe wa Kundi la Wataalamu waliopelekwa kuchunguza namna vikwazo vinavyotekelezwa kuenedelza shughuli zao bila pingamizi. Azimio limetaka huduma za Kundi la Wataalamu ziendelezwe nchini kwa mwaka mmoja zaidi.

Hali ya mapigano Usomali inatisha na ni ya hatari

Christian Balslev-Olesen, Mshauri Mkazi kwa Huduma za Kiutu Usomali aliwasilisha hadharani barua maalumu iliofafanua hali ya vurugu katika Usomali. Balslev-Olesen aliwatahadharisha viongozi wa Usomali na makundi yote husika na hali huko, ikijumuisha vikosi vya Ethiopia, kwamba wanawajibika, kwa kulingana na sheria za kiutu za kimataifa, kuheshimu haki za raia na wajitahidi kuchanganua ni nani raia na nani mpiganaji wakati wanapoendeleza operesheni zao.

KM amemtuma mjumbe maalumu katika JKK kusaka amani

KM Ban Ki-moon ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kwa hali ya uhasama na mapigano katika jimbo la mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK). Alisema anakhofia athari zake huenda zikafurika eneo la Maziwa Makuu na kusababisha hali ya mtafaruku na vurugu dhidi ya usalama na utulivu wa amani wa umma.

Hapa na pale

UM, ikishirikiana na makampuni ya kimataifa ya Googles na Cisco, yenye kuongoza katika taaluma na teknolojia za ,awasiliano ya kisasa yameanzisha kipamoja anuani mpya ya mtandao itakayompatia mtumiaji kompyuta fursa ya kufuatilia, kihakika, namna miradi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) inavyotekelezwa na kuendelezwa katika maeneo mbalimbali ya dunia. ~