Skip to main content

Hali ya mapigano Usomali inatisha na ni ya hatari

Hali ya mapigano Usomali inatisha na ni ya hatari

Christian Balslev-Olesen, Mshauri Mkazi kwa Huduma za Kiutu Usomali aliwasilisha hadharani barua maalumu iliofafanua hali ya vurugu katika Usomali. Balslev-Olesen aliwatahadharisha viongozi wa Usomali na makundi yote husika na hali huko, ikijumuisha vikosi vya Ethiopia, kwamba wanawajibika, kwa kulingana na sheria za kiutu za kimataifa, kuheshimu haki za raia na wajitahidi kuchanganua ni nani raia na nani mpiganaji wakati wanapoendeleza operesheni zao.

Mjumbe huyu wa UM alipendekeza kwa makundi hayo wawache tabia karaha ya kuhujumu mastakimu ya raia, na vile vile kuwataka wawahakikishie mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu kuwa watapatiwa fursa halali ya kuendeleza kadhia zao bila ya vitisho wala pingamizi. Alionya kwamba mapigano ya karibuni nchini Usomali yamesababisha mgogoro mkubwa kabisa dhidi ya utu. Ripoti za UM zinaelezea kwamba kuanzia tarehe 27 hadi 29 Oktoba karibu watu 90,000 walihajiri mji wa Mogadishu na walikimbilia mji wa Afgooye ambapo wakitarajia kupatiwa misaada ya kihali, eneo ambalo tangu mwanzo limeghumiwa na jukumu kubwa la kuhudumia kihali wahamiaji wengineo wa ndani ya nchi ziada 100,000.