Waandaji filamu Kenya, Tanzania na Uganda ni miongoni mwa washindi wa awali wa shindano la UNESCO na Netflix
Waandaaji watano wa filamu kutoka Afrika Mashariki ni miongoni mwa waaandaji filamu 21 kutoka barani Afrika ambao wamepita katika mchujo wa awali wa shindano la shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO pamoja na kampuni ya kutengeneza na kusambaza filamu, Netflix la kutengeneza filamu za hadithi za kiafrika.