Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kuhakikisha ufugaji samaki Zimbabwe una tija shambani hadi mezani

Samaki waliovuliwa kwenye shamba la samaki la familia kufuatia mfumo wa umwagiliaji unaovuta maji kutoka mto ulio jirani.
UN Photo/Logan Abassi
Samaki waliovuliwa kwenye shamba la samaki la familia kufuatia mfumo wa umwagiliaji unaovuta maji kutoka mto ulio jirani.

FAO kuhakikisha ufugaji samaki Zimbabwe una tija shambani hadi mezani

Ukuaji wa Kiuchumi

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema ingawa teknolojia ya ufugaji wa Samaki nchini Zimbabwe imekua bado lengo la kufanikisha uhakika wa chakula kwa kuhakikisha Samaki anafika mezani bado linakabiliwa na changamoto kwa kuwa gharama ya ufugaji ni ya juu halikadhalika gharama ya kitoweo hicho.