ILO Afrika Mashariki yaungana na wenyeji kusherehekea siku ya wafanyakazi
Leo ni siku ya wafanyakazi duniani, au Mei mosi ambapo mataifa ikiwemo yale ya barani Afrika yameadhimisha siku hiyo huku shirika la kazi ulimwenguni ukanda wa Afrika Mashariki likitoa wito kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuchagiza usawa, haki kwa jamii na kuimarisha mazingira ya kazi kwa wote.