
Mamia ya maelfu ya watu walikimbilia kusini kutoka kaskazini mwa Gaza. OCHA inakadiria kuna takriban watu milioni moja waliokimbia makazi yao wakiwemo zaidi ya 353,000 wanaojihifadhi katika shule za Shirika La Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu kama lile la Mpango wa Chakula WFP yamekuwa yakisambaza mikate na misaada mingine kwa wakimbizi, lakini chakula kinamalizika.
© UNICEF/Hassan Islyeh

Siku ya Ijumaa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari kwamba kuwezesha misaada kuingia Gaza kupitia kivuko cha Rafah ni sawa na “tofauti kati ya uhai na kifo.”
UN Photo/Eskinder Debebe