
Vyombo vya habarikutoka kila kona ya duniani navyo vilirejea kwa wingi kuandikisha mikutano ya kilele, matukio ya kando, hotuba na mikutano katika kumbi mbalimbani ndani ya Umoja wa Mataifa wakati ambao ni wiki yenye shughuli nyingi zaidi katika Umoja wa Mataifa.

Kila Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa anapata fursa ya kupanda jukwaani katika Ukumbi wa Mkutano Mkuu na kutoa hotuba.
Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine alitoa hotuba yake ya kwanza ana kwa ana kwenye Umoja wa Mataifa tangu nchi yake kuvamiwa na Urusi.

Uwepo wa viongozi wakuu wa Umoja wa Mataifa katika hafla za SDG, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed pichani hapa, ulisisitiza umuhimu wa kusaidia Nchi Wanachama kufikia Malengo.

Suala jingine lililoangaziwa ni athari za Mabadiliko ya Tabianchi na baadhi ya jamii zilizoathiriwa zaidi ulimwenguni zilitoa maoni yao. Pia, jambo la kwanza, wale walioalikwa kuzungumza walitakiwa kuonesha mipango inayoaminika ya kupunguza hewa chafuzi zinazosababisha ongezeko la joto duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alihudhuria mikutano mingi na kukutana na viongozi kadhaa wa kimataifa.