MINUSMA ilitumwa nchini Mali mwaka 2013 kufuatia uasi mkali wa waasi wanaotaka kujitenga wakijaribu kuchukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo na kufuatia na mapinduzi ya kijeshi.
Miongoni mwa kazi kuu za MINUSMA ilikuwa ni pamoja na kusaidia mpito wa kisiasa na kulinda raia.
UN Photo/Marco Dormino
Mkuu wa Kitengo cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix (wa pili kutoka kulia), alitembelea misheni hiyo mara nyingi. Katika picha alienda kuhani wafanyakazi wenzake waliopoteza maisha wakati wakitekeleza kazi yao ya linda amani na kuwatambua kazi kubwa inayofanywa na walinzi wote wa amani “ambao wanahudumu kwa ajili ya amani bila ubinafsi”.
MINUSMA/Harandane Dicko