
Jevanic Henry, mjumbe wa Kundi la Ushauri la Vijana la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mawaziri katika HLPF. Kulia ni Asma Rouabhia akiwakilisha Bunge la vijana linalojikita na SGD7.

Nathalie Chuard (katikati), Mkurugenzi wa Kituo cha DCAF huko Geneva Uswisi kinachohusika na Utawala wa Sekta ya Usalama, akizungumza katika mkutano wa kando kuhusu Kuharakisha Utekelezaji wa SDG 16 katika kuunga mkono maendeleo endelevu na kudumisha amani.
Pia waliopo katika picha ni Maritza Chan (kushoto), Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Costa Rica katika Umoja wa Mataifa, na Brian J. Williams (kulia), Mkuu, Ufadhili wa Tawi la Kujenga Amani, UN DPPA.

Taasisi na mashirika ya kiraia na asasi kutoka kila kona ya dunia nazo zinashirika katika mkutano huu wa HLPF na miongoni mwa shughuli wanazofanya ni maonesho ya shughuli zao huko mashinani.
Katika picha ni Bezawit Girma kutoka shirika la ASEZ WAO linalojihushisha na vijana kujitolea kutekeleza SDGs akitoa maelezo ya shirika hilo kwa Whitney Kennedy anayehudhuria HLPF.

Sio asasi na mashirika ya kiraia pekee yanayofanya maonesho wa shughuli wanazozifanya za kutekeleza SDGs, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa nao wametengewa maeneo maalumu ya kufanya maonesho.
Katika picha ni meza ya maonesho ya Tanzania ambapo maafisa wake wanaonesha shughuli wanazozifanya nchini mwao katika kuhakikisha wanatekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs kabla ya kufika mwaka 2030.