![Timu ya wahudumu wa afya wa kliniki tembezi ikiingia eneo la vijijini, wilayani Mueda jimboni Cabo Delgado. Timu ya wahudumu wa afya wa kliniki tembezi ikiingia eneo la vijijini, wilayani Mueda jimboni Cabo Delgado.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/Libraries/Production%20Library/28-01-2024_UNFPA_Mozambiqu_Cabo_Delgado_Mobile_Clinic_Mueda.jpg/image770x420cropped.jpg)
Wahudumu wa afya wa kliniki tembezi husafiri kwa njia ya nchi kavu au baharini ili kuwafikia wanawake na wasichana wanaoishi katika maeneo ya vijijini na visiwani jimboni humo, ambao vinginevyo wanaweza kukosa huduma ya afya kama vile afya ya ngono na uzazi. Wakati wa mvua maeneo haya hayafikiki.
![Ancha (kushoto) akipokea dawa za kuongeza dawa za kuongeza damu mwilini kutoka kwa Juliana Germano ndani ya kliniki tembezi ya UNFPA. Ancha (kushoto) akipokea dawa za kuongeza dawa za kuongeza damu mwilini kutoka kwa Juliana Germano ndani ya kliniki tembezi ya UNFPA.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/Libraries/Production%20Library/28-01-2024_UNFPA_Mozambiqu_Cabo_Delgado_Iron_Ancha.jpg/image770x420cropped.jpg)
Ancha akiwa amebeba mwanae mwenye umri wa miaka mitatu amefika kliniki na anapatiwa dawa za virutubisho vya madini ya chuma ili kuongeza damu mwilini kutoka kwa muuguzi Juliana Germano wa AMODEFA katika kliniki tembezi. Dawa hizo huepusha mwanamke kupata tatizo la ukosefu wa damu.
![Juliana Germano, mtaalamu wa afya kutoka Chama cha maendeleo ya familia Msumbiji, (AMODEFA) ndani ya kliniki tembezi. Juliana Germano, mtaalamu wa afya kutoka Chama cha maendeleo ya familia Msumbiji, (AMODEFA) ndani ya kliniki tembezi.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/Libraries/Production%20Library/28-01-2024_UNFPA_Mozambiqu_Cabo_Delgado_Checkup_Rufina.jpg/image770x420cropped.jpg)
Juliana Germano wa AMODEFA akimpima mjamzito Rufina. Huduma hizi zinazotolewa na UNFPA hapa Cabo Delgao zinasaidia kupunguza hatari ya kujifungua mapema, kuepusha maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na vifo vya uzazi na ukatili wa kijinsia.
![Elena, mwenye umri wa miaka 15, wakati wa kikao cha kupatiwa ushauri na mwanaharakati wa jamii Zaida, katika wilaya ya Metuge jimboni Cabo Delgado. Elena, mwenye umri wa miaka 15, wakati wa kikao cha kupatiwa ushauri na mwanaharakati wa jamii Zaida, katika wilaya ya Metuge jimboni Cabo Delgado.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/Libraries/Production%20Library/28-01-2024_UNFPA_Mozambiqu_Cabo_Delgado_Counselling.jpg/image770x420cropped.jpg)
Hapa ni kituo rafiki kwa wanawake na wasichana wilayani Metuge, jimbo la Cabo Delgado na mwanaharakati wa kijamii Zaida (kulia) akimpatia ushauri wa nasaha mtoto wa kike Elena mwenye umri wa miaka 15. Mazungumzo kama haya yanasaidia kuepusha ngono zisizo salama na mimba zisizotarajiwa.