UNMISS yapatia mafunzo wafanyabiashara Sudan Kusini ili wafanye biashara kwa ufanisi
Ushirikiano na ukuaji kiuchumi ni miongoni mwa masuala muhimu katika kuhakikisha nchi yoyote ina amani na wananchi wake wanapata Maendeleo. Na ili kuhakikisha wananchi wa Sudan Kusini wana amani na maendeleo, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani nchini humo UNMISS umeandaa warsha ya biashara lengo likiwa ni kuwatia moyo wafanyabiashara wa ndani na kuwawezesha kiuchumi ili nao waweze kuimarisha biashara zao lakini pia waweze kufanya biashara na Umoja wa Mataifa .