Mlipuko wa 12 wa Ebola Kivu Kaskazini umetokomezwa - WHO
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO hii leo kupitia taarifa iliyotolewa mjini Brazzaville Congo na Kinshasa, DRC, limetangaza kumalizika kwa mlipuko wa 12 wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, miezi mitatu tu baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa Kivu Kaskazini.