Mkutano wa kirafiki wakutanisha walinda amani kutoka Tanzania na baadhi ya viongozi mashariki mwa DRC
Kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na katika kuendeleza jukumu la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vikosi vya ulinzi wa amani kutoka Tanzania yaani TANZBATT 9 na kikosi cha utayari TANZANIA QRF2 vimefanya kikao cha Urafiki baina yao na uongozi wa raia wa nchi hiyo katika maeneo ya uwajibikaji wa vikosi hivyo.