Nuru Burundi kwa haki za jamii ya Watwa
Mkutano wa 21 wa Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, UNPFFII likiwa limeingia siku ya tatu kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, washiriki kutoka Burundi wameieleza Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa juu ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha haki za binadamu za jamii ya asili aina ya watwa zinazingatiwa.