Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Lori likiwa limejaa chupa za maji ya kunywa  likielekea Al Arish mji ulio kilometa 32 kusini mwa mpaka wa Gaza
© UNICEF/Mohamed Ragaa

Udadavuzi: Kuna nini ndani ya msafara wa misaada kwenye kivuko cha Gaza

Chini ya kilomita moja kutoka Gaza, vibao vya kuengeshean chakula, mafuta, maji, na dawa ni miongoni mwa mamia ya tani za misaada ya kuokoa maisha iliyopakiwa kwenye msafara mrefu wa malori yakiwa yamesimama kwenye upande wa Misri wa kivuko cha mpakani ch a Rafah, huku madereva wakisubiri ruksa ya Israel ili waweze kufikia Wapalestina milioni 2.3 waliozingirwa na walionaswa katika mzozo wa vita vinavyoendelea.

Jengo liliporomoka huko Gaza.
© UNRWA/Mohammed Hinnawi

Mgogoro Mashariki ya Kati: Umoja wa Mataifa unasaidia vipi?

Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi katika eneo la Mashariki ya Kati muda wote ili kupunguza mzozo wa Israel na Palestina kwa kuwashirikisha wahusika wakuu na kutoa msaada wa dharura kwa raia walioko mashinani. 

Wakati mzozo huo ukiongezeka huku kukiwa na ongezeko la ghasia, kizuizi kamili cha chakula, maji, na huduma muhimu kiliwekwa na Israel huku ripoti zikiibuka kuhusu operesheni za ardhini za Israel huko Gaza, ambako kuna wakazi zaidi ya milioni mbili.