Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

01 MACHI 2024

01 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 unaokunja chamvi leo, na utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO kuhusu utipwatipwa. 

  1. Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 umefunga pazia leo jijini Nairobi, Kenya baada ya siku 5 za majadiliano na shughuli mbalimbali zilizohusisha zaidi ya wajumbe 7,000 kutoka Nchi 182 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo amekuwa akizungumza na washiriki mbalimbali kuhusu walivyonufaika na mkutano huo na hapa ni mmoja wao kutoka jamii za wafugaji ambao duniani kote mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri moja kwa moja.
  2. Utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO unaonyesha kwamba, mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanaishi na unene wa kupindukia ama utipwa tipwa. Duniani kote, unene wa kupindukia kwa watu wazima umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1990, na umepanda mara nne kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19. 
  3. Makala inaturejesha kwenye mkutano wa UNEA6 ambapo Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano mbalimbali kwa lengo la kuisogeza dunia mahala bora zaidi katika upande wa mazingira. Stella Vuzo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS hakuachwa nyuma amekuwa akizungumza na wadau mbalimbali wanaoshiriki mkutano huo wa UNEA6 tangu ulipoanza na leo yuko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa Tanzania Dkt. Selemani Jafo na kwanza amemuuliza anachokibeba kutoka kwenye mkutano huo.”
  4. Na mashinani tunamsikia binti Muthoni Truphena, kiongozi wa kikundi cha watoto wanaharakati wa mazingira nchini Kenya ambao wanachochea mabadiliko chanya katika jamii zao wakiungwa mkono na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, anapazia sauti kizazi chake katika mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 jijini Nairobi.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'41"