Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 JUNI 2023

30 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana nchini Sudan na kazi ya walinda amani nchini CAR. Makala tutakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Misri, kulikoni?

  1. Wanawake  na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao.
  2. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR (MONUSCO) wametoa mafunzo ya upishi kwa vikindi vya wanawake wa Kijiji cha Moro kilichoko takribani kilometa 50 kutoka Mji wa Berberati, jimboni Mambere Kadei yalipo makao makuu ya kikosi hicho.   
  3. Makala tunakupeleka nchini DRC ambapo Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu.
  4. Katika mashinani na leo tutaelekea nchini Misri ambapo wanawake waliokimbia migogoro nchini Sudan kuelekea nchini humo wanapokea huduma za afya ya akili baada ya kupitia machungu.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
13'4"