Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Misri

Rosemary DiCarlo akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama kuhusu shambulio la Israel Doha Qatar
UN Photo/Loey Felipe

Shambulio la Israel Doha Qatar laleta mshtuko, UN yataka diplomasia iheshimiwe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo lilipewa taarifa na afisa mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu shambulio la anga la Israel mjini Doha Qatar na kusema ni ongezeko la kutisha la mvutano lililolaaniwa kama uvunjaji wa mamlaka ya nchi unaotishia mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka huko Gaza.

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, amezitaka mamlaka za Misri kukomesha utaratibu unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kutumikia vifungo vyao au kukamilisha muda wa juu wa kizuizi cha…
© UNODC/Laura Gil

Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN yatoa wito kwa Misri kukomesha utaratibu wa kionevu wa “mzunguko”

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo Jumanne ya Agosti 26 jijini Geneva, Uswisi ametoa wito kwa mamlaka za Misri kukomesha utaratibu unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kutumikia vifungo vyao au kukamilisha muda wa juu kabisa wa kizuizi cha kabla ya kesi.

Msaada wa elimu kwa wakimbizi wa Sudan walioko Kusini mwa Misri.
UN News

Upungufu wa ufadhili wawaweka wakimbizi wa Sudan nchini Misri hatarini: UNHCR

Mgogoro wa kimataifa wa ufadhili wa misaada ya kibinadamu umelilazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR, kusimamisha huduma muhimu za kuokoa maisha kwa wakimbizi nchini Misri, na kuwaacha maelfu ya watu, wakiwemo wakimbizi wa Sudan, bila matibabu muhimu na huduma za ulinzi kwa watoto, imesema taarifa iliyotolewa na Leona shirika hilo mjini Cairo, Misri.

Watoto wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza wakiwa na taa kusherehekea mwezi tukufu wa Ramadhani.
© UNRWA

Mkuu wa UN aanza ziara ya mshikamano kipindi cha Ramadani huko Misri na Jordan

Kutokana na kuongezeka kwa mizozo na migogoro ya kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameanza safari yake ya kila mwaka ya mshikamano kipindi cha Ramadhani, inayoanza wikendi hii mjini Cairo, Misri. Safari hiyo ambayo inasadifiana na mwezi mtukufu wa Ramadhani, inafanyika katika nyakati za misukosuko hasa kutokana na mzozo unaoendelea huko Gaza.