02 APRILI 2020
Katika Jarida la habari hii leo assumpta Massoi anakuletea
-Siku ya uelimishaji kuhusu usonji ikiadhimishwa leo Umoja wa Mataifa umetoa wito kuhakikisha watu hao wanajumuisha katika harakati za kupambana na janga la virusi vya Corona , COVID-19
-Huko nchini Suda Kusini japo bado hakuna mgonjwa yeyote wa virusi vya Corona COVID-19 mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS kwa kushirikiana na serikali wachukua hatua kujikinga ikiwa ni pamoja na kufunga soko kubwa mpkani wa nchi hiyo na DRC
-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema liko katika maandalizi makubwa kwenye kambi ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan ya zaa'tar kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 endapo utatokea kambini hapo
-Makala yetu leo inatupeleka nchini Tanzania ambako madereba wa usafiri wa pikipiki maarugu kama Bodaboda wanachukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kusaga ndoo na sabuni kwa ajili ya kunawa mikono
-Na mashinani ikiwa ni siku ya kuelimisha jamii kuhusu usonji, tunakwenda Tanzania kukutana na mshairi Glory Titus Moshi almaarufu GloryPoetry.