Ukame uliofuatiwa na mafuriko watishia uhakika wa chakula Sri Lanka

Ukame uliofuatiwa na mafuriko watishia uhakika wa chakula Sri Lanka

Pakua

Hali mbaya ya ukame iliyofuatiwa na mvua kubwa iliyoleta mafuriko nchini Sri Lanka imeathiri uzalishaji wa mazao, na kutishia uhakika wa chakula kwa takribani watu 900,000 kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la chakula na kilimo FAO na lile la mpango wa chakula duniani WFP.

Hali hiyo iliyokithiri mwaka 2016 na mapema 2017 imeathiri zaidi kilimo cha mpunga. Cristina Coslet, ni mchumi katika shirika la FAO

(SAUTI YA CRISTINA)

“Ukame ulioikumba Sri Lanka mwaka 2016 na mapema 2017 ulikuwa ni mbayaza azidi katika kipindi cha miaka 40, ukame huo umepunguza upatikanaji wa maji katika kipindi upanzi cha mahar na matokeo yake uzalishaji wa mazao umepungua kwa kiasi cha asilimia 40 na hata zaidi katika baadhi ya maeneo.”

Photo Credit
Uharibifu uliyosababishwa na mafuriko nchini Sri Lanka. Picha: IOM