Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na Wambui Kahara-mwakilishi wa vijana kutoka Kenya

Mahojiano na Wambui Kahara-mwakilishi wa vijana kutoka Kenya

Pakua

Kamati ya tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ikihitimisha mjadala wa vijana kuhusu maendeleo ya jamii, idhaa hii imeongea na mwakilishi kutoka Kenya, Wambui Kahara ambaye ameeleza jinsi Kenya ilivyojitahidi kuwawezesha vijana katika uchumi wa nchi.

Amesema ingawa maswala ya malengo ya maendeleo ni "maneno makubwa" kwa vijana wengi, ni muhimu washirikishwe ili wamiliki utaratibu huo, huku akitoa pia ujumbe kwa vijana wote waliopo Afrika ya Mashariki. Kumsikia zaidi, ungana na Priscilla Lecomte kwenye mahojiano haya.

Photo Credit
Wambui Kahara-mwakilishi wa vijana kutoka Kenya. Picha: Priscilla Lecomte