Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Amminadab Jean

Siyo ulemavu wote unaonekana-Wataalam wa Afya

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya walemavu na kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa “sio ulemavu wote unaonekana” ni bayana kuwa  watu wengi duniani wanaishi na ulemavu wa aina fulani ambao hauonekani ambao wakati mwingine unaweza kuchukuliwa kuwa labda tabia zao na hata watu hao kukumbwa na unyanyapaa katika jamii. Mara nyingi ulemavu unaozingatiwa huwa ule unaonekana kwa mfano ulemavu wa miguu, mikono au macho ingawa nao bado wanakumbana na changamoto nyingi.

Sauti
3'46"
© World Bank/Sarah Farhat

Vijana wapeana mawaidha ya kuepuka ghasia mandamanoni, Uganda

Karibu kote duniani vijana hua msitari wa mbele kwneye mandanmano na vilevile kukumbana na matokeo yake ikiwemo vifo, kujeruhiwa na kufungwa jela.

Kawaida sababu ni ukosefu wa ajira na kutaka nafasi kwenye uongozi ingawa mara nyingine baadhi yao hutumikishwa tu bila wao wenyewe kuwa na sababu ya msingi.

Je, ni jinsi gani kijana binafsi yaweza kujizuia kushiriki kwneye mandamano yasio halali na ya ghasia? Je, kwa nini vyombo vya usalama hutumia nguvu kupita kiasi.

Sauti
3'58"
UN Tanzania/Nafisa Didi

Nilitaabika na UKIMWI na sitaki wenzangu wataabike kama mimi- Bi. Masao.

Katika maisha ya binadamu, uzoefu unaonesha kuwa ni nadra kumkuta kiumbe apendaye kuepusha mwenzake kutopitia mabaya yaliyomkumba. Lakini si kwa Hellen Thomas Masao, mwalimu mstaafu nchini Tanzania ambaye anasema kubainika kuwa na Virusi vya Ukimwi, ilikuwa ni kama tiketi ya kifo, lakini mola alimuepusha na sasa anatumia uzoefu wake kuhakikisha walimu wenzake wa umri wake na vijana hawapitii unyanyapaa aliopitia yeye hadi ameanzisha taasisi ya kusaidia walimu wanaoishi na VVU, TAPOTI.

Sauti
5'21"