Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wapeana mawaidha ya kuepuka ghasia mandamanoni, Uganda

Vijana wapeana mawaidha ya kuepuka ghasia mandamanoni, Uganda

Pakua

Karibu kote duniani vijana hua msitari wa mbele kwneye mandanmano na vilevile kukumbana na matokeo yake ikiwemo vifo, kujeruhiwa na kufungwa jela.

Kawaida sababu ni ukosefu wa ajira na kutaka nafasi kwenye uongozi ingawa mara nyingine baadhi yao hutumikishwa tu bila wao wenyewe kuwa na sababu ya msingi.

Je, ni jinsi gani kijana binafsi yaweza kujizuia kushiriki kwneye mandamano yasio halali na ya ghasia? Je, kwa nini vyombo vya usalama hutumia nguvu kupita kiasi.

Basi tuelekee nchini Uganda ambako John Kibego ameandaa makala akiangazia nafasi ya vijana na msimamo wao na serikali katika kukabiliana na wandamanaji wakati huu wa kampeni za kisiasa zilizoghubikwa na vuta nivute juu ya vizuizi vya kudhibiti COVID-19.

Audio Credit
Anold Kayanda/ John Kibego
Audio Duration
3'58"
Photo Credit
© World Bank/Sarah Farhat