Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilitaabika na UKIMWI na sitaki wenzangu wataabike kama mimi- Bi. Masao.

Nilitaabika na UKIMWI na sitaki wenzangu wataabike kama mimi- Bi. Masao.

Pakua

Katika maisha ya binadamu, uzoefu unaonesha kuwa ni nadra kumkuta kiumbe apendaye kuepusha mwenzake kutopitia mabaya yaliyomkumba. Lakini si kwa Hellen Thomas Masao, mwalimu mstaafu nchini Tanzania ambaye anasema kubainika kuwa na Virusi vya Ukimwi, ilikuwa ni kama tiketi ya kifo, lakini mola alimuepusha na sasa anatumia uzoefu wake kuhakikisha walimu wenzake wa umri wake na vijana hawapitii unyanyapaa aliopitia yeye hadi ameanzisha taasisi ya kusaidia walimu wanaoishi na VVU, TAPOTI.

Mwelekeo ni kufanikisha azma ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha kuwa mwishoni mwa mwaka huu wa 2020 kunakuwepo uwiano wa 90-90-90 yaani asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wafahamu hali yao, asilimia 90 ya wanaobainika kuwa na VVU wapate matibabu na asilimia 90 ya wanaopata madawa ya kufifisha VVU, virusi hivyo viwe vimefifishwa. Ni kwa kutambua mchango wake, Nafisa Didi, afisa habari wa kituo cha Habari za UN jijini Dar es salaam nchini Tanzania, UNIC alizungumza na Mwalimu Masao huko Moshi, kilimanjaro kunakofanyika maadhimisho ya siku ya Ukimwi kitaifa na kisha Ahimidiwe Olotu wa UNIC kuandaa makala hii, kwako Ahimidiwe!

Audio Credit
Anold Kayanda/ Hellen Thomas Masao
Audio Duration
5'21"
Photo Credit
UN Tanzania/Nafisa Didi