Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi na adha ya kusaka huduma

Kuelekea mkutano wa ngazi ya juu kuhusu masuala ya wakimbizi na wahamiaji duniani, utakaofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani, mwandishi wetu nchini Uganda, John Kibego amefuatilia madhila wanayokumbana nayo wakimbizi na wahamiaji nchini humo wakati serikali nayo ikihaha kuwapatia makazi na huduma za kijamii. Mathalani baadhi ya watu wa kabila la jamii la Alur, wenye asili ya Uganda wanaonekana kuwa ni wakongo, na hivyo kukumbwa na madhila wanaposaka huduma. Hayo ni mengine mengi ameyafafanua katika makala hii.

Ronaldinho na udau wa Umoja wa Mataifa

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linatambua umuhimu wa kushirikisha ulimwengu wa michezo, kwani michezo ndio njia rahisi ya kupenya katika mioyo ya watoto na watu wazima duniani kote. Ushirikiano huu unasaidia UNICEF katika kupigia chepuo haki za watoto kucheza, kuwasilisha ujumbe maalum, kuhamasisha jamii na muhimu zaidi, kuhakikisha maendeleo endelevu ya watoto , familia na jamii. Moja ya timu inayoshirikiana na UNICEF ni FC Barcelona ya Hispani, na katika makala hii tunamulika ujumbe wao wakati wa ziara yao hapa kwenye Umoja wa Mataifa.

Harakati za kisomo nchini Tanzania

Kisomo! Yaani kujua kusoma na kuandika ni suala linaloelezwa kuwa ni kitovu cha mafanikio ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Katika siku ya kimataifa ya kisomo wiki hii, Umoja wa Mataifa umetaka hatua zichukuliwe kuimarisha kisomo kwa watu wazima, vijana na watoto. Hii ni kwa sababu miaka 50 tangu kuanza kuadhimishwa kwa siku hiyo, watu zaidi ya milioni 750 hivi sasa ulimwenguni kote hawajui kusoma na kuandika.Nchini Tanzania hatua zinachukuliwa na Nicholous Ngaiza wa radio washirika wa radio washirika Kasibante FM mkoani Kagera, anaangazia hali iko vipi mkoani humo.

Hatua za Uganda kwa wakimbizi zamshangaza mkuu wa UNHCR

Sudan Kusini, mzozo ulioanza mwezi Disemba mwaka 2013 umesababisha maelfu ya raia kukimbilia nchi jirani ikiwemo Uganda. Hivi karibuni, Kamishana Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filipo Grandi alizuru kambi ya wakimbizi ya muda wa Nyumanzi kaskazini mwa Uganda, lengo la ziara ikiwa ni kutathmini jinsi hali yalivyo kambini humo na jinsi maafisa wa Umoja wa Mataifa wanavyoendesha shughuli yao. Je hali ilikuwaje? ungana basi na Briann Lehander katika makala hii.