Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Balozi mwema Kipchumba ahaha kutokomeza Polio Kenya

Harakati za kupambana na ugonjwa wa Polio duniani zinashika kasi kila uchao licha ya changamoto zinazokumba watoa huduma ya chanjo hiyo. Mathalani katika baadhi ya maeneo, watoa huduma hukumbwa na vikwazo vya imani za wananchi husika.

Wengine wao huamini kuwa kwa kusali tu, basi ugonjwa huoutatokomea. Nchini Kenya, katika kaunti ya Kitui, kanisa moja lina imani hiyo. Kwa kutambua madhara ya Polio, Seneta Harold Kipchumba kutoka Kenya ambaye ni balozi mwema wa UNICEF  kutokomeza Polio nchini humo  amefunga safari hadi eneo hilo kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo.

Ulemavu wa ngozi si kikwazo chochote kwangu- Keisha

Jina Keisha ni maarufu si tu nchini Tanzania ambako mwanamuziki huyo wa kike anaendesha shughuli zake za muziki, bali pia sasa limetambuliwa na wataalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Kisa? ni jinsi mwanamuziki huyo alivyoruka viunzi vya ubaguzi na hata kutovitambua na kuendelea na maisha yake.

Juhudi za kutokomeza Ukimwi duniani #HLM2016AIDS

Mkutano wa ngazi ya juu wa siku tatu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu namna ya kukomesha maambukizi ya Ukimwi umfungwa Ijumaa mjini New York.

Huu ni mkutano uliowaleta pamoja, mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia, wanaharakati wa makabiliano dhidi ya Ukimwi, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine.

Hatua zimepigwa katika mapambano dhidi ya ukimwi,juhudi zaidi zahitajika:Dr Kigwangalla

Serikali ya Tanzania imesema imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya ukimwi, lakini mafanikio hayo hayatakuwa na maana endapo watabweteka. Hayo yamesemwa na naibu waziri wa afya wan chi hiyo Dr Hamis Kigwangalla alipoketi na kuzungumza na Flora Nducha wa idhaa hii.

Pia amesema changamoto kubwa waliyonayo ni rasilimali fedha, sasa wameunda mkakati kabambe kuhakikisha wanazipata na kusukuma mbele mchakato wa kufikia lengo la kutokomeza ukimwi ifikapo mwaka 2030 kama sehemy ya utekelezaji wa maendeleo endelevu yaani SDG’s.

UN Photo/Abel Kavanagh

MONUSCO yaimarisha uwezo wa polisi katika doria DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani MONUSCO kinaimarisha uwezo wa polisi wa nchi hiyo katika kuhakikisha amani na usalama wa mipaka na raia.

Katika operesheni maalum ziwani, MONUSCO wanafanya operesheni ya mfano. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

Mkutano wa polisi umetujenga kuimarisha usalama DRC: IGP Bisengimana

Mwishoni mwa juma lililopita, wakuu wa polisi kutoka kote duniani walikutana hapa New York kujadili nafasi ya polisi katika ulinzi wa amani. Bara la Afrika hususani nchi za Maziwa Makuu ziliwakilishwa vyema.

Joseph Msami wa idhaa hii amefuatilia mkutano huo na kuzungumza na mkuu wa jeshi la polisi kutoka Jamhuri ya Kidemokraia ya Kongo DRC Charles Bisengimana anayeanza kueleza umuhimu wa mkutano huo.

Mabadiliko ya tabianchi na hatua za kukabaliana nayo Tanzania

Mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania sasa ni dhahiri! La muhimu ni kuchukua hatua za kukabilaina nazo. Hizo ni sauti za wakazi wa Kagera nchini humo ambao wanasema mfumo wa maisha yao ikiwamo kipato na ustawi wao kwa ujumla umeathirika pakubwa.

Katika makala ifuatayo, Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe Fm anakusimulia jinsi wilaya ya Karagwe ilivyoathirika na hatua zinazochukuliwa. Ungana naye.

UNICEF yawapatia nuru watoto wakimbizi Tanzania

Nchini Tanzania, idadi ya wakimbizi kutoka Burundi imefika 138,000, wengi wao wakiwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF, maelfu miongoni mwao hawakuambatana na mzazi au mlezi yeyote.

UNICEF kwa ushirikiano na mashirika mengine inawasaidia watoto hao kupata familia za kuwalea na kuwapatia matumaini upya.