Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Miaka 70 ya UM Tanzania, yapo mengi ya kujivunia:

Mwaka 1945 Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa malengo mahsusi ikiwemo kuendeleza amani na usalama duniani, kuchagiza maendeleo endelevu na kutetea haki za binadamu.

Miaka 70 tangu kuanzishwa kwake, chombo hicho chenye wanachama 193 hivi sasa kimeendelea kusimamia malengo hayo na matunda yako dhahiri kwa nchi wanachama ikiwemo Tanzania.

Je nini Umoja wa Mataifa imefanya katika taifa hilo lililoko Afrika Mashariki? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Maelfu ya wakimbizi kutoka Yemen wanatarajiwa kuwasili Djibouti

Hali ya kibinadamu nchini Yemen inazidi kuzorota kwa kasi, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatarajia kuwa katika miezi michache ijayo zaidi ya wakimbizi 30,000 kutoka Yemen watawasili pwani ya Djibouti na wengine 100,000 nchi jirani ya Somalia.

Hii ni kutokana na mzozo wa wenyewe kwa wenyewe ulioshamiri baada ya kuanza kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Houthi.

Je waliokimbia Yemen na sasa wanaishi ugenini maisha yako vipi? Ungana na Joseph Msami kwenye makala hii..

Utafiti wa dawa ni baadhi ya mbinu za kutokomeza malaria Kenya

Katika kukabiliana na malaria nchini Kenya mbinu mbadala zimekuwa zikitumika mathalani utafiti na mbinu shirikishi ili kutimiza lengo la kuwa na jamii isiyo na maambukizi ya malaria ugonjwa unaosababishwa na mbu aina ya anophlex ambako takwimu za mwaka jana zinaashiria kwamba takriban watu milioni 15 waliambukizwa ugonjwa huo.Basi ungana na Geoffrey Onditi wa radio washirika KBC katika makala hii,  anayeanza kwa kuzungumza na wanananchi ili kufahamu uelewa wao kuhusu malaria.

Ukosefu wa ajira unaathiri jamii asilia hususani vijana

Vijana wa kimaasai huathirka sana kwa kukosa kazi na wanatumbukia katika majanga kama vile kuuza madawa ya kulevya, ni kauli ya mwakilishi wa jamai ya kimasaai kutoka Tanzania aliye pia mwakilishi wa shirika la maendeleo ya wanawakwe wamaasai MWEDO, Ndinini Kimesirasika.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa  idhaa  hii kandoni mwa kongamano la 14 la watu wa asili linaloendelea mjni New York Bi Ndinini amesema pia jamii hizo zinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa elimu. Kwanza anaanza kueleza ujumbe wa  MWEDO  katika kongamano.

Matumizi mabaya ya dini sasa yaangaziwe: Balozi Koki

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki hii kumefanyika mjadala kuhusu stahamala na maelewano baina ya watu wa imani tofauti za kidini. Washiriki walikuwa viongozi wa dini mbali mbali pamoja na wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Kenya ambao walieleza uzoefu wao katika harakati za vita dhidi ya ugaidi wakati huu ambapo vinahusishwa na matumizi mabaya ya dini. Je nini uzoefu wa Kenya na katika mjadala huo wamejifunza nini?

Stahamala katika dini muarobaini wa machafuko

Dunia ikiwa inashuhudia matukio ya kigaidi na machafuko  yanyotokana na chuki sehemu mbalimbali, makundi yanayojihusisha na ugaidi na machafuko mengine yamekuwa yakitumia mwavuli wa dini katika kuhasisha na hata kutekeleza mashambulizi.

Umoja wa Mataifa kwa kutambua hilo umekutana na viongozi mbalimbali wa dini duniani hapa makao makuu mjini New York. Nini kimejiri? Ungana na Priscilla Lecomte katika makala ifuatayo

Kufunguliwa kwa shule baada ya Ebola kwaibua furaha Sierra Leone

Baada ya kadhia ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliosababisha vifo ya maelfu ya watu, katika nchi za Afrika ya Magharibi hususan Liberia, Sierra Leone na Guinea, shule ambazo zilifungwa awali ili kuepuka maambukizi zaidi zimefunguliwa.

Nchini Sierra Leone kufunguliwa kwa shule hizi kumeibua furaha kwa wadau mbali mbali wa elimu.

Basi ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

Dawa mseto bado ni thabiti dhidi ya Malaria Tanzania:

Zaidi ya asilimia 93 ya watanzania wanaishi kwenye  maeneo ambayo yanawaweka hatarini kukumbwa na Malaria. Hata hivyo serikali ya Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua za kinga, tiba na utambuzi wa mapema ili kudhibiti kuenea kwa Malaria. Je ni hatua gani zimechukuliwa wakati huu wa kuelekea siku ya Malaria duniani tarehe 25 Aprili.? Assumpta Massoi wa idhaa hii amezungumza na Dkt. Renata Mwandike, Naibu Meneja wa mpango wa kitaifa wa kudhibiti Malaria nchini humo ambapo hapa ameanza kwa kuelezea matokeo ya utafiti kuhusu maambukizi ya Malaria miongoni mwa watoto.