Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Tafiti zaidi zahitajika kubaini kiwango cha ukatili wa kijinsia: TAMWA

Siku ya wanawake duniani ni fursa ya kutathmini hatua zilizochukuliwa kulinda hadhi na ustawi wa mwanamke na mtoto wa kike. Nchini Tanzania, chama cha waandishi wa habari wanawake, TAMWA kiliendesha utafiti kubaini kiwango cha ukatili wa kijinsia, utafiti uliofanyika katika wilaya Kumi nchini humo. Je nini kilibainika? Na matokeo ya utafiti huo yanalenga kuboresha nini? Basi ungana na Stella Vuzo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam Tanzania katika mahoajiano yake na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valeri Msoka. Valerie anaanza kwa kutaja wilaya husika.

UNMISS yatoa elimu juu ya kazi na wajibu wa ujumbe huo Sudan Kusini

Katika kutoa elimu juu ya wajibu na majukumu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) katika jamii ya jimbo la Jonglei, ujumbe huo ulizuru jamii ya watu wa AKUIDENG BOMA, mji ulioko Jalle Payam takribani kilometer 60 kutoka mji unaofahamika kama Bor.

Ungana na Joseph Msami katika makala hii inayomulika juhudi za UNMISS katika kuwaelimisha raia namna ya kushirikiana na ujumbe huo kukomesha mapigano na kuleta amani ambayo imekuwa ni adimu nchini Sudan Kusini, taifa lililozaliwa mwezi Julai mwaka 2011.

UNICEF na washirika wasaidia waathirika wa Kipindupindu Haiti

Haiti nchi iliyoko katika visiwa vya Karibia ni nchi ambayo imekumbwa na ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu .Hii inatokana na majanga mbalimbali ya kibinadamu kama vile matetemeko ya ardhi yaliyosababisha watu wengi kukosa makazi na hivyo kuishi katika mazingira hatarishi.

Mlipuko wa kipindupindu umechangiwa na mikusanyiko ya watu katika nyumba zisizo rasmi, yakiwemo mahema, huku pia sababu nyingine inayotajwa kuchangia ugonjwa huo unaodhoofisha na kuua haraka ni misongamano mikubwa ya nyumba na matumizi mabaya ya huduma za kijamii kama vile maji na hata vyakula.