Kituo cha Afya na vifaa vya matibabu vyaharibiwa na vikundi vinavyojihami huko Tambura Sudan Kusini
Licha ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya amani nchini Sudan Kusini mwaka 2018, mapigano bado yanaendelea katika maeneo tofauti tofauti nchini humo ikiwemo mji wa Tambura jimboni Equatoria Magharibi na hivyo kukwamisha harakati za kufikisha huduma za matibabu na wakimbizi wa ndani kuzidi kutaabika.
(Taarifa ya Leah Mushi)
Video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS inaanza kwa taswira ya uharibifu katika kituo cha afya mjini Tambura, uharibifu uliofanywa na vikundi vilivoyjihami