Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Ukiukaji wa haki za binadamu DRC umeongezeka asilimia 30: UM

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour ameesema ukiukaji wa haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Bwana Gilmour meyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea huko Geneva, Uswis akiongeza kuwa ukiukwaji huo ni kuhusiana na kuzuia demokrasia na kuanza tena kwa shughuli za makundi kadhaa yenye silaha.

Bado kuna mapungufu makubwa katika kukabiliana na haki za binadamu Guinea: UM

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour akizungumza kwenye kikao cha haki za binadamu katika mjadala kuhusu Guinea, amesema licha ya ahadi ya serikali baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya mwisho ya mashauriano ya kitaifa ya Juni 29 kuweka kipaumbele katika mapambano dhidi ya uonevu, bado kuna mapungufu makubwa katika kukabiliana na matukio mengi.

Ukosefu wa maji Pangani waleta mtafaruku wa ndoa na jamii

Ukosefu wa maji wilayani Pangani huko mkoani Tanga nchini Tanzania sio tu kwamba unahatarisha afya za wakazi wa wilaya hiyo, bali pia unasababisha mafarakano miongoni mwa wanajamii wanadoa na kuzorotesha maendeleo.

Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo anaangazia adha hiyo inayokupa visa na mikasa ikiwamo kukesha kusubiri maji huku mama mmoja akisimulia namna mmewe alivyomwaga maji yake aliyoyateka . Kulikoni? Ungana naye.

Hali ya kibinadamu yazidi kuzorota Somalia-UM

Wakati tishio la baa la njaa likizidi kunyemelea Somalia, hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota nchini humo, umesema Umoja wa mataifa Jumatano. Takribani watu 257,000 wametawanywa nchini Somalia tangu Novemba 2016 hadi Februari mwaka huu, huku wengine zaidi ya elfu nne wakivuka mpaka kuingia Ethiopia .

Ombi la msaada halijafikia hata nusu na gonjwa la kipindupindu na kuhara vikizidi kutishia maisha ya maelfu kama anavyofafanua msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini New York

(Sauti ya Farhan)

Takriban watoto milioni 600 wataishi kwenye uhaba wa maji ifikapo 2040-UM

Takriban watoto milioni 600 au 1 kati ya 4 kote duniani wataishi katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa maji ifikapo mwaka 2040 kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF iliyotolewa Jumatano  katika siku ya maji duniani.

Ripoti hiyo ‘kiu kwa siku za usoni:maji na watoto katika mabadiliko ya tabia nchi” inaangalia vitisho kwa maisha ya watoto na mustakhbali wao vinavyosababishwa na kupungua kwa rasilimali ya maji na njia ambazo mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha hatari hiyo katika miaka ijayo.

Kikosi cha kikanda kuwasili Sudan Kusini- Ladsous

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kikosi cha kikanda cha ulinzi kitaanza kuwasili Sudan Kusini wiki chache zijazo, ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Baraza la Usalama la umoja huo.

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema hayo leo huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini alikokuweko ziarani kwa siku mbili baada ya ziara kama hiyo nchini Mali.

Mvutano wa nani awe Waziri Mkuu DRC ndio kikwazo- Ripoti

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejulishwa utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, bado umekwama, ikiwa ni miwili tangu yatiwe saini.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kuhusu DRC, ripoti iliyowasilishwa na mwakilishi wake maalum nchini DRC, Maman Sambo Sidikou.

(Sauti ya Maman)