Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa maji Pangani waleta mtafaruku wa ndoa na jamii

Ukosefu wa maji Pangani waleta mtafaruku wa ndoa na jamii

Pakua

Ukosefu wa maji wilayani Pangani huko mkoani Tanga nchini Tanzania sio tu kwamba unahatarisha afya za wakazi wa wilaya hiyo, bali pia unasababisha mafarakano miongoni mwa wanajamii wanadoa na kuzorotesha maendeleo.

Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo anaangazia adha hiyo inayokupa visa na mikasa ikiwamo kukesha kusubiri maji huku mama mmoja akisimulia namna mmewe alivyomwaga maji yake aliyoyateka . Kulikoni? Ungana naye.

Photo Credit
Uhaba wa maji husababisha wanawake kupoteza muda mwingi iwe bombani au kisimani. (Picha:© UNICEF Tanzania/2015/Beechey)