Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Tuna matumaini na mjadala wa kitaifa nchini Gabon - UM

Wakati Gabon inajiandaa na mjadala wa kitaifa kesho Jumanne, Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kwa Afrika ya kati, UNOCA, Francois Louncény Fall amesema wana imani kubwa kuwa mjadala huo utaendeshwa kwa amani, utulivu na utakuwa jumuishi.

Taarifa ya UNOCA imesema kwa miezi miwili sasa Bwana Fall ameimarisha juhudi za kufanya majadiliano na wadau mbalimbali nchini Gabon ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali, upinzani, vyama vya kiraia, vijana na wanawake.

UNESCO yazindua kitabu cha mwongozo waandishi wa habari za ugaidi

Shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO limezindua kitabu cha mwongozo kwa waandishi wa habari ili kuongeza uelewa wao zaidi katika kuandika habari kuhusu ugaidi.

Taarifa ya UNESCO imesema kitabu hicho kilichoandikwa na Jean-Paul Marthoz kitawezesha wanahabari kutekeleza majukumu yako ya kuhabarisha umma bila kuwapatia fursa magaidi ya kufanikisha lengo lao la kugawa wananchi.

Mathalani wawe makini ni nani wanamnukuu na ni ujumbe gani wanaotoa licha ya shinikizo kutoka kwa wasomaji, watazamaji na wasikilizaji.

Maktaba/UN

Harakati za kutokomeza nyuklia zaanza, nchi 40 zasema hazitoshiriki

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeanza awamu ya kwanza ya mkutano wake wa kujadili mbinu yenye nguvu kisheria ambayo itawezesha kutokomeza silaha za nyuklia ulimwenguni.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa kikao hicho kitakachomalizika tarehe 31 mwezi huu, balozi Elayne Whyte Gomez wa Costa Rica amesema amani ni lazima iibuke mshindi dhidi ya silaha za nyuklia.

(Sauti ya Elayne)

“Tunapaswa kuongozwa kwa mashauriano na siyo kutokupatana. Tunapaswa kuongozwa na maafikiano na si uzembe.”

UN Photo/Evan Schneider

Uchumi wa Zambia unakua lakini yahitaji marekebisho ya sera- IMF

Shirika la fedha duniani, IMF limesema Zambia imechukua hatua ili kuwezesha shirika hilo kusaidia mipango ya uchumi.

IMF imesema hayo kufuatia ziara ya wiki mbili nchini humo iliyoongozwa na Tsidi Tsikata.

Mathalani imetaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na mipango ambamo kwayo inahakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo na kiuendelevu pamoja na malipo ya malimbikizo ya madeni ya umma bila kulundika mengine.

Bwana Tsikata amesema kwa hatua hizo, uchumi wa Zambia unatarajiwa kukua kidogo kwa asilimia 3.5 mwaka huu wa 2017.

Viongozi Sudan Kusini zingatieni amani- Mahamat

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU, Moussa Faki Mahamat yuko nchini Sudan Kusini ambako ametoa wito wa utekelezaji wa mkataba wa amani ili kumaliza machungu yanayokabili wananchi.

Akizungumza huko Ganyiel, kwenye jimbo la Unity Kusini, Bwana Mahamat amesema kiwango cha machungu ni cha kupitiliza na zaidi ya yote janga la kibinadamu.

Amesema aliguswa na kile alichoshuhudia na kutoa wito kwa pande husika katika mzozo kuhakikisha kuna amani ili taifa hilo liweze kurejea katika hali ya kawaida.

Licha ya juhudi za kimataifa , milio ya risasi na mabomu yaendelea kunguruma Yemen:O’Brien

Licha ya juhudi za kimataifa za kuleta suluhu ya kudumu ya kisasa Yemen, milio ya makombora, mabomu, risasi na vifaru sasa imekuwa ada katika maisha ya kila siku nchini humo.

Hayo yamesema na Stephen O’Brien msaidizi wa Katibu mkuu katika masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, katika taarifa yake kuhusu miaka miwili baada ya kuzuka machafuko Yemen.

Amesema maelfu ya raia wameuawa, wakiwemo wasichana na wavulana zaidi ya 1400, wengi wa watoto hao walitoka majumbani kwao kuelekea shuleni na hawakurejea tena, huku raia wengine kwa maelfu wakijeruhiwa.

Vita vikiingia mwaka wa pili familia Yemen zageukia hatua kujikimu: UNICEF

Baada ya miaka miwili ya vita, familia nchini Yemen zinageukia hatua kali ili kukidhi mhitaji ya watoto wao, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika ripoti yake iliyotolewa Jumatatu.

Ripoti inasema njia za kujikimu zimesambaratishwa na machafuko na kuigeuza Yemen kuwa moja ya nchi zenye tatizo kubwa la uhakika wa chakula na dharura ya utapia mlo duniani.

KNCCI yanufaisha wanawake wafanyabiashara Kenya

Chama cha wafanyabiashara na wenye Viwanda nchini Kenya, KNCCI, kimesema kimepatia kipaumbele wanawake upande wa biashara na sasa asilimia 90 ya wanufaika wameweza kuinua jamii zao.

Naibu Mwenyekiti wa chama hicho Rukia Rashid amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani.

Amesema mipango ya usaidizi ni pamoja na kuunganisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa tofauti na kwamba..

(Sauti ya Rukia)

Hata hivyo amesema licha ya mafanikio, kuna changamoto.

(Sauti ya Rukia)