Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Buba waendelea kushambulia watoto duniani: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema ugonjwa wa buba ambao hushambulia zaidi watoto bado unazishambulia nchi 13 duniani, licha ya shirika hilo kutangaza mwaka jana kuwa  India haina tena ua.

Taarifa ya shirika hilo kuhusu ugonjwa huo inasema kuwa matibabu yake ni rahisi kwani dozi moja pekee ya kunywa ya dawa iitwayo kwa kitaalamu azithromycin, yatosha kuponya buba.

WHO imesema inawezekana kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, ikiwa tu dawa hiyo inapatikana na hilo laweza kutekelezwa ifikapo mwaka 2020.

UN Photo - Jean-Marc Ferre

Uikukwaji na ukatoili mkubwa unaendelea Libya:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Jumanne kwamba imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, sheria za kimataifa za binadamu na ukatili kutoka pande zot e za mzozo tangu kuzuka tena kwa uhasama Machi 3 mwaka huu.

Ofisi hiyo inasema habari za kuaminika zinaeleza kwamba mauaji ya kinyume cha sheria ikiwemo ya kiholela, utekaji, watu kuzuiliwa kizuizini , utesaji na msako dhidi ya nyumba za raia vimekuwa vikifanyika hasa katika miji ya Ajdabiya, Benghazi, Brega na Beishir.

Ukame umeyaweka rehani maisha ya watoto Somalia-UM

Magonjwa yanayohusiana na ukame yamekatili maisha ya watoto 47 katika miiezi miwili iliyopita katika moja ya hospitali inayoendeshwa na serikali mjini Mohadishu Somalia. Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSE)

Umoja wa Mataifa umetoa onyo kwa dunia kwamba athari za ukame ukichanganya na vita katika taiafa hilo la Pembe ya afrika zinaweza kuwa zahma kubwa, kwani takriban watu milioni tatu wako katika hatari ya baa la njaa.

Mashambulizi mawili ya bomu yakatili maisha ya waSyria 40

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani mauaji ya watu zaidi ya 40 na kujeruhi wengine katika milipuko miwili ya mabomu yaliyotokea Jumamosi katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa,  wengi wa wale waliouawa walikuwa wasafiri ambao walikuwa wakisafiri kwa basi kwenda katika makaburi takatifu, ambalo hutembelewa zaidi na kundi lingine la kiisilamu lijulikanalo kama Shiite.

Simulizi ya wanawake Afghanistan itabadilika wakishiriki kwenye uongozi - UNAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao chake kuhusu Afghanistan ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Tadamichi Yamamoto amesema katika nusu ya kwanza ya kipindi cha serikali ya umoja wa kitaifa, tayari hatua za maendeleo zimepigwa licha ya changamoto zinazotakiwa kupatiwa suluhu siku zijazo.

Ametaja maeneo matatua ambayo yameonyesha matumaini kuwa ni  pamoja na kupambana na rushwa, mchakato wa uchaguzi na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Wakimbizi Kigoma waadhiimisha siku ya wanawake

Maadhimisho ya siku ya wanawake nchini Tanzania yamefanyika sehemu mbalimbali licha ya kwamba kitaifa yamefanyika mkoani Singida.

Mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, mvua kubwa iliyonyesha awali haikuwazuai wananchi kujitokeza kuhudhuria maadhimisho hayo yaliyotia fora kwa burudani na ujumbe. Tuungane na Mabamba Mpela Junior

Burudani zasheheni wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Wanawake wameshamiri juma hili. Mataifa mengi yameadhimisha siku ya wanawake duniani mnamo Machi nane, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka, lengo likiwa kupigia chepuo haki na ustawi wa kundi hilo katika nyanja mbalimbali.

Katika makala ifuatayo Assumpta Massoi anamulika namna burudani ilivyotumiwa kufikisha ujumbe hususani nchi zenye mizozo, huku ikiwaliwaza washiriki, wakiongozwa na wanawake ambao ni walengwa.