Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uikukwaji na ukatoili mkubwa unaendelea Libya:UM

Uikukwaji na ukatoili mkubwa unaendelea Libya:UM

Pakua

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Jumanne kwamba imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, sheria za kimataifa za binadamu na ukatili kutoka pande zot e za mzozo tangu kuzuka tena kwa uhasama Machi 3 mwaka huu.

Ofisi hiyo inasema habari za kuaminika zinaeleza kwamba mauaji ya kinyume cha sheria ikiwemo ya kiholela, utekaji, watu kuzuiliwa kizuizini , utesaji na msako dhidi ya nyumba za raia vimekuwa vikifanyika hasa katika miji ya Ajdabiya, Benghazi, Brega na Beishir.

Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geveneva Uswiwi anasema  makundi mawili makubwa yenye silaha yanapigania udhibiti wa eneo la mashariki lenye mafuta.

Amesema kwa sasa ni jeshi la kitaifa la Libya (LNA) na kikosi cha ulinzi cha Beganzi (BDB) Machi tatu BDB na wafuasi wake walishambulia eneo la mafuta na kuchukua udhibiti kutoka kwa LNA , na LNA wakaanza kujibu mashambulizi katika eneo hilo kwa njia ya anga

Imearifiwa kwamba wanaume na wavulana Zaidi ya 100 walikamatwa wakati wa msako wa LNA, na jeshi hilo liliwapiga na kuwatusi wana ume na wanawake huku likiwaibia fedha na vitu vingine majumbani kwao.

Photo Credit
UN Photo - Jean-Marc Ferre