Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN Photo/OCHA/David Ohana

Wakati Walibya wakikimbilia Ulaya, wengine wahamia nchini kwao: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema leo kuwa, wakati maelfu ya raia wa Libya wakikimbia nchi yao kusaka hifadhi mataifa ya Ulaya, asilimia 81 hadi 83 ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika ikiwamo Misri, Chad na Sudan wananuia kuhamia Libya .

Taarifa ya IOM inasema hali ni tofauti kwa raia wa Nigeria ambao ni asilimia 16 tu wenye nia ya kusalia nchini humo wakati ambapo asilimia 43 ya raia hao wanakusudia kuendelea kusafiri kuelekea Italia.

Taarifa hiyo inasema kuwa asilimia 12 wananuia kwenda Ujerumani na asilimia iliyosalia katika mataifa mengine barani Ulaya.

Kunyonyesha watoto ni haki ya binadamu: UM

Umoja wa Mataifa umesema kunyonyesha watoto ni suala la haki za binadamu kwa watoto na akina mama na linapaswa kulindwa na kupgiwa chepuo kwa faida ya wote.

Katika taarifa ya pamoja ya wataalamu huru wa UM, wameyataka mataifa kuchukua hatua za dharura kukomesha upotoshaji unofanywa na kampuni za kibiashara kuhusu unyonyeshaji mbadala usiozingatia misingi ya afya.

Wataalamu hao wamesema upotoshaji huo hufanywa na viwanda vya maziwa ambavyo huzalisha mabilioni kupitia ushawishi huo.

Picha na UM

Mswada Bungeni Uturuki kuwapa msamaha wanyanyasaji wa watoto

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la idadi ya watu UNFPA, kitengo kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women na lile la mpango wa maendeleo UNDP nchini Uturuki, wana wasiwasi na mswada wa mapendekezo utakaowasilishwa bungeni wakati wa mijadala ya kisheria iliyoanza tangu Novemba 17 ambayo inaweza kusababisha baadhi ya aina ya msamaha kwa unyanyasaji wa watoto kwa masharti kwamba wahusika watawoa wathirika.

Shambulio la kigaidi lililoua 32 Afghanistan limelaaniwa na UM

habariunamaShambulio la kigaidi nchini Afghanistan lililokatili maiasha ya raia 32 mjini Kabul, limelaaniwa vikali na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekluwa amevaa vifaa vya mlipuko amejilipua kwenye msikini wa Baqer-ul Jumatatu ambako waumini Kiislam wa Kishia walikuwa wamekusanyika kuadhimisha arbadeen sherehe za siku ya 40 baada ya Ashura.

Mabadiliko katika ngazi zote yanahitajika kwa kuleta usawa wa kijinsia kazini:UNDP

Mabadiliko yanahitajika katika ngazi zote katika jamii ili kuboresha hali ya usawa wa kijinsia makazini , kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa. Wataalamu kutoka kila kona ya dunia wamekusanyika Panama Jumatatu kwenye kongamano la tatu la biashara kuhusu usawa wa kijinsia linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Kongamano hilo litajikita katika jinsi gani sekta binafsi inaweza kuweka mazingira ya usawa na kujenga mazingira ya kazi jumuishi. Randi Davis, ni mkurugenzi wa timu ya masuala ya jinsia kwenye shirila la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

Uvuvi unaingiza dola bilioni 135 kila mwaka:FAO

Sekta ya uvuvi kimataifa inaingiza wastani wa dola bilioni 135 kwa mwaka kama mapato ya usafirishaji nje wa vidhaa zake, limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Sekta hiyo pia inatoa ajira au kipato kwa mtu mmoja kati ya 10 duniani huku pia ikiwa chanzo kikubwa cha asilimia 17 ya vyakula vya kujenga mwili au ptotini vinavyoliwa kote duniani.

Akizungumza katika mkutano maalumu ulioandaliwa na FAO na Holy kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na uvuvi haramu katika sekta ya uvuvi, mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema sekta za uvuvi

UNESCO yalaani mauaji ya mwanahabari DRC

Mkurugenzi Mkuu wa shirik,a la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, Irina Bokova, leo amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Televisheni, Marcel Lubala wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, yaliyofanyika kati ya kati ya 14-15 Novemba mjini Mbuji-Mayi, nchini humo

Kupitia taarifa yake, Bi Bokova amesema wanahabarui wanapaswa kufanya kazi zao ya kutaarifu umma bila hofu ya maisha yao, n akuongeza kuwa anatarajia mamalaka nchini humo itanendesha uchunguzi na wahusika watafikishwa katika vyombio vya sheria.

Zaidi ya watu 3400 hupoteza maisha kila siku kwa ajali za barabarani:

Vijana ndio wahanga wakubwa wa ajali za barabarani kuliko watu wazima limesema shirika la afya ulimwenguni WHO.

Katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kila siku watu zaidi ya 3400 wanapoteza maisha barabarani kote duniani sawa na watu karibu milioni 1.3 kwa mwaka.