Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Dansi, mavazi na nyimbo zatamalaki siku ya wafanyakazi wa UM

Wiki hii Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya wafanya kazi wa Umoja huo. Wafanyi kazi katika sehemu mbali mbali kuliko ofisi za Umoja wa Mataifa wameadhimisha siku hii kwa njia mbali mbali. Hapa makao makuu wafanyakazi wamefanya hafla maalum kwa ajili ya kuenzi vipaji vya wafanyakazi wake, hafla ya mwisho kufanyika ilikuwa muongo mmoja uliopita na hivyo maadhimisho hayo yamekaribishwa huku wafanyakazi wakishiriki kwa njia mbali mbali ikiwemo kuvaa mavazi ya kitamaduni, kucheza dansi, kughani mashairi na pia kuimba.

Ban alaani shamulio dhidi ya shule Aleppo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi dhidi ya shule mashariki mwa mji wa Aleppo nchini Syria hii leo ambayo yamesababaisha vifo vya watu kadhaa.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu, imemnukuu Ban akisema matuko kama mashambulizi hayo yamefanywa kwa kukusudia yaweza kuchochea uhalifu wa kivita.

Amesema wahusika wa vitendo hivyo lazima wafikishwe katika mkono wa sheria na kusisistiza wito wake kwa Baraza la Usalama kupelekea suala la Syria katika mahakama ya kimtaifa ya uhalifu, ICC.

Umoja wa Mataifa na uwezeshaji vijana nchini Tanzania

Oktoba 24 ni siku ya Umoja wa Mataifa ambapo chombo hicho chenye nchi wanachama 193 huangazia shughuli zake zinazojikita katika misingi mikuu ya maendeleo, Amani na usalama na haki za binadamu. Kuelekea siku hiyo, Umoja wa Mataifa huandaa shughuli mbali mbali ikiwemo wiki ya vijana, ambayo lengo kuu ni kuchagiza vijana hasa wakati huu ambapo ushiriki wao ni muhimu ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Watoto Calais wamo hatarini:UNICEF

Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema limesikitishwa mno na matukio ya jana usiku ambapo watoto wakimbizi wamelazimika kulala nje kwenye baridi baada ya kambi yao kuteketezwa moto huko Calais, Ufaransa. Halikadhalika, UNICEF imeshtushwa pia na habari zingine za watoto kutosajiliwa na kupewa vitambulisho na hivyo kurudishwa na polisi kambini.

UN Photo/Evan Schneider

Wakimbizi wapya na wa muda mrefu wahitaji msaada

Watoa misaada ya kibinadamu wanatupia jicho kwa karibu hali ya wakimbizi waliosahaulika na wa muda mrefu, lakini pia wakimbizi wapya katika ngazi ya kimataifa kwa lengo la kushughulikia changamoto zinazowakabili watu hao ambao kutwa wako safarini.

Hayo yamesemwa na mshauri maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu kushughulikia suala la wakimbizi na wahamiaji Karen AbuZayd. Nchi zilipitisha azimio la New York mwezi Septemba ili kulinda na kuokoa maisha ya wakimbizi na wahamiaji.

Ndege zisizo na rubani zawezesha miradi ya ardhi Tanzania

‘Ni teknolojia rahisi, isyohitaji rubani’. Hii ni kauli ya mmoja wa maafisa wa serikali ya Tanzania wakati akielezea namna ndege zisizo na rubani au Drones zinavyowezesha umilikishwaji wa ardhi, kupanga miji na hata kukabiliana na mafuriko.

Ungana an Jospeh Msami katika makala inayoeleza mradi huu unaofadhiliwa na benki ya dunia unavyonufaisha taifa hilo la Afrika Mashariki.

ICC ichunguze hima mauaji ya watoto 22 na walimu sita Syria: Brown

Mauaji dhidi ya watoto 22 na walimu sita huko Idlib nchini Syria ni uhalifu wa kivita dhahiri mauaji hayo yanapaswa kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua na mahakama kimataifa ya uhalifu ICC.

Hayo ni kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu Gordon Brown ambaye amezungumza na waandishi wa habari mjini New York hii leo.

Bwana Brown ambaye ameonyesha dhahiri kusononeshwa na tukio hilo amesema.

( SAUTI BROWN)

Wamakonde wasio na uraia Kenya hatimaye wapewa vitambulisho

Hatimaye watu wenye asili ya Kimakonde 6,000 sasa wataondokana na tatizo la kutokuwa na utaifa baada ya serikali ya Kenya kuwatambua na kuwapa vitambulisho, limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR .

Kwa mujibu wa shirika hilo watu hawa ambao wazazi na babu zao waliwasili nchini Kenya mwaka 1936 kutoka Tanzania na Msumbiji, walikuja kufanya kazi katika mashamba ya katani na miwa na hawakurudi nyumbani, na kwa miaka mingi sasa wamenyimwa haki zao za msingi za kibinadamu, kwani hawakutambuliwa kama raia wa Kenya.