Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN Photo/Eskinder Debebe)

Akiwa DRC, Ban akutana na Kabila, ahimiza ushirikiano na MONUSCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ambaye yuko ziarani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DCR, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo.

Taarifa ya msemaji wake imesema kuwa, wakati wa mkutano wao, Katibu Mkuu amehimiza serikali ya DRC kuendelea kufanya mazungumzo ya kimkakati na ujume wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, pamoja na kubuni mkakati wa kuondoka kwa ujumbe huo nchini DRC.

Sudan Kusini yazindua ripoti ya kwanza ya maendeleo ya binadamu

Serikali ya Sudan Kusini na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP wamezindua ripoti ya kwanza kabisa ya hali ya maendeleo ya kibinadamu nchini humo.

Ripoti hiyo imezinduliwa wakati taifa hilo changa zaidi duniani likikabiliwa na changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii huku likihaha kusaka mbinu za kujikwamua.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo yenye maudhui, Watu, Amani na Ustawi Naibu Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa Sudan Kusini Eugene Owusu amesema..

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari Ufilipino

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amelaani vikali mauaji ya mwandishi wa habari kutoka Ufilipino, Elvis Ordaniza, ambaye ameuawa tarehe 16 Februari kwenye eneo la Mindanao, Ufilipino, kwa kupigwa risasi.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na UNESCO Bi Bokova ameomba uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji hayo.

Ameongeza kwamba waandishi wa habari wanapaswa kuwa na haki ya kufanya kazi zao kwa usalama, akizisihi mamlaka za serikali kufanya lolote liwezekanalo ili kupeleka watekelezaji wa uhalifu huo mbele ya sheria.

Vunjeni mzunguko wa ukimya na kukubali ukatili dhidi ya wanawake:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake, sababu na athari zake Dubravka Šimonović leo amekaribisha maendeleo muhimu katika sheria za Georgia kuhusu usawa wa kijinsia na ukatikli dhidi ya wanawake, lakini ameonya kwamba mabadiliko makubwa zaidi yanahitajika katika mtazamo wa jamii dhidi ya ukatili wa kijinsia ikiwemo unyanyasaji majumbani na ndoa za mapema.

Angalau DPRK sasa inasikiliza Baraza la Haki- Balozi Choi

Rais wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Balozi Kyong-lim Choi amesema kutokomeza ukiukwaji wa haki za binadamu huko Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK, Burundi na Syria ni miongoni mwa vipaumbele vya vikao vya baraza hilo vinavyoanza Jumatano ijayo.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi, Balozi Choi ambaye ni mara ya kwanza anashika wadhifa huo amesema nchi hizo ni kati ya 47 zitakazoangaziwa utendaji wake wa haki za binadamu ambapo ukiukwaji wa haki unaleta majanga.

Watu wa Syria wanahitaji kuona tofauti katika hali yao sasa- O’Brien

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu Katika Umoja wa Mataifa, Stephen O’Brien, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kuwa mzozo wa Syria hauwezi kutatuliwa iwapo hali ya kutowalinda kabisa raia nchini humo itaendelea.

Akikumbusha kuwa watu wa Syria wameteseka kwa muda mrefu, na kwamba mzozo huo utakuwa umedumu kwa miaka mitano mwezi ujao, Bwana O’Brien amesema jamii ya kimataifa imekuwa ikitizama tu, huku mzozo huo wa Syria ukizidi kuwa mkubwa zaidi na wenye uharibifu mkubwa zaidi katika kizazi cha sasa

Mjini Goma, Ban akutana na mkombozi wa wanawake, Daktari Mukwege

Akiwa ziarani mashariki mwa DRC, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na Daktari Denis Mukwege, ambaye ni mkuu wa hospitali ya Panzi Kivu Kusini inayoshughulikia kutibu na kupasua wanawake walioathirika na ubakaji nchini humo.

Akizungumza na Bernardin Nyangi wa Redio ya Umoja wa Mataifa, Radio OKAPI baada ya mazungumzo ya ana kwa ana na Katibu Mkuu, Daktari Mukwege amesema mafanikio makubwa yalipatikana katika juhudi za kupambana na ubakaji kwenye maeneo ya Kivu, kwa ushirikiano na wadau mbali mbali na Umoja wa Mataifa.

Kuwekeza katika kuzuia migogoro kuna gharama ndogo kuliko kuitatua- Balozi Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Macharia Kamau, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Ujenzi wa Amani, amesema leo kuwa kuwekeza katika kuzuia mlipuko wa mzozo kuna gharama ndogo na ni endelevu zaidi kuliko jitihada za kukabiliana na mizozo tu.

Balozi Kamau amesema hayo wakati wa mjadala wa wazi katika Baraza la Usalama, ambao umehusu kufanyia tathmini mfumo wa ujenzi wa amani, ambapo ameeleza umuhimu wa kamisheni hiyo anayosimamia

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Homs na Damascus,Syria

Wajumbe wa Baraza la Usalama, wamelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa katika miji ya Homs na Damscus nchini Syria, mnamo Februari 21, ambayo yaliwaua watu 130 na kujeruhi mamia ya wengine.

Kundi la kigaidi linalotaka kuweka dola la uislamu wenye itikadi kali (ISIL/Da’esh) limedai kutekeleza mashambulizi hayo.

Wajumbe wa Baraza la Usalama wametuma salamu za rambirambi na faraja kwa familia za wahanga, na kwa watu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria, huku wakiwatakia uponaji wa haraka waliojeruhiwa.