Redio hukwamua watu katika majanga Burundi
Nchini Burundi redio inatajwa kuwa chombo muhimu cha mawasiliano wakati wa majanga, mathalani wakati wa mafuriko ambayo hivi karibuni pia yameikumba nchi hiyo.
Nchini Burundi redio inatajwa kuwa chombo muhimu cha mawasiliano wakati wa majanga, mathalani wakati wa mafuriko ambayo hivi karibuni pia yameikumba nchi hiyo.
Nchini Tanzania siku ya Jumatano kumefanyika kongamano la wadau wa harakati za kukabiliana na tatizo la madawa ya kulevya.
Kufuatia miezi ya kuzuiwa kuufikia mji wa Taiz nchini Yemen, Shirika la Afya Duniani hatimaye limeweza kufikisha tani 20 za dawa za kuokoa maisha na vifaa tiba vingine kwa mji huo, katika jitihada za kushughulikia mahitaji yanayoongezeka ya dharura ya afya.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo FAO José Graziano da Silva amesema FAO iko tayari kuchangia katika jitihada za kukabiliana na dharura ya kiafya ya virusi vya Zika.
"Nikiona nyembe au vitu vyenye ncha kali nakumbuka nilivyokeketwa”Ni kauli ya manusura wa mila potofu ya ukeketaji kutoka Kenya Keziah Oseko ambaye amekutana na mwandishi wa idhaa hii Joseph Msami kandoni mwa mkutano kuhusu kupinga kitendo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu madawa na uhalifu (UNODC), Yuri Fedotov, amesema leo kwamba, haiwezi kukubalika kuwa huenda watoto wahamiaji 10,000 wasio na wazazi au walezi wametoweka wakiwa safarini kwenda Ulaya, na kutaka hatua za dharura ichukuliwe kimataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la leo la shirika la masuala ya anga duniani, ICAO la kupendekeza viwango vya uchafuzi vinavyotolewa na vyombo vya usafiri angani ikiwemo ndege.
Radio, imeendelea kuwa mwokozi wakati wa majanga kwa kuwapatia wananchi taarifa sahihi za jinsi ya kujiokoa. Mathalani nchini Tanzania mwaka 2014 katika mkoa wa Mbeya kusini mwa nchi hiyo, mafuriko yalikumba wakazi wa wilaya ya Kyela na kusababisha uharibifu wa mali.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezindua ripoti yake kuhusu kongamano la kimatiafa la masuala ya kibinadamu litakalofanyika mwezi Mei mwaka huu huko Uturuki akisema binadamu wote wanawajibika kupunguza mateso ya mamilioni ya watu na kukabiliana na changamoto zinazoikumba dunia.
Nchini Syria, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limeanza kusambaza vyakula kwa watu waliolazimika kuhama makwao kaskazini mwa Aleppo kufuatia kuongezeka kwa mapigano kwenye eneo hilo.