Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabrasha la Sauti

15 NOVEMBA 2022

Leo katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa tunakuletea Habari kwa Ufupi zikimulika idadi ya watu kufikia bilioni 8, Mada kwa Kina tunakupeleka Peru kumulika wanawake wa jamii ya asili na upandaji miti, na Mashinani tunamulika polisi wa Umoja wa Mataifa na ulinzi wa amani.

Sauti
12'12"
Eric Omondi, muuguzi wa Kituo cha Usimamizi na Taarifa za Kisukari anakagua eneo lenye uvimbe kwenye mkono wa Maingi.

Wagonjwa wengi wa Kisukari barani Afrika hata hawajitambui- WHO

Wakati dunia ikiadhimisha hii leo siku ya kisukari duniani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti tishio lake, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa

Sauti
3'43"
WFP/Falume Bachir

Wakazi wa Cabo Delgado nchini Msumbiji hatihati kukosa misaada ya binadamu iwapo WFP haitapatiwa fedha za nyongeza

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema iwapo halitapokea fedha za nyongeza, litalazimika kusitisha msaada muhimu wa kibinadamu kwa wakazi milioni moja wa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ifikapo kilele cha msimu wa njaa mwezi Februari mwakani kutokana na ukata

Sauti
2'39"