WHO yatoa tani 70 ya vifaa vya Hispitali Yemen
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO, limepeleka tani 70 za misaada ya kibinadamu ikiwemo vifa upasuaji kwajili ya hospitali katika mji mkuu Sana huko Yemen.
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO, limepeleka tani 70 za misaada ya kibinadamu ikiwemo vifa upasuaji kwajili ya hospitali katika mji mkuu Sana huko Yemen.
Nchini Somalia wiki hii wamezindua sera ya taifa ya vijana ambayo kwayo inazungumzia hatua za kukwamua vijana kuelekea utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.
Ghana kuweni macho na kampuni binafsi za ulinzi ambazo siyo tu idadi yao imeongezeka kama uyoga bali pia zinaweka upenyo wa askari mamluki.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na kilimo FAO, na la mpango wa chakula WFP yamekusanya nguvu ili kukabiliana na tatizo la njaa katika eneo la Kasai Kuu huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.
Mila za baadhi ya makabila katika bara la Afrika, zimesheheni changamoto za unyanyapaa kwa wajane wanapodai au kupigania mali za waume zao. Mara nyingi wanawake hao huishia kunyanganywa kila kitu na ndugu wa marehemu na kusababisha mgawanyiko katika familia.
Hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea kuighubika syria leo imetawala kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo maafisa wanaoshughulikia suala la kisiasa na kibinadamu nchini humo wametoa tarifa.
Mwaka 2017 umekuwa ni mwaka mgumu zaidi kwa maisha ya wanawake na watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR/
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya habari na teknolojia ya mawasiliano ITU limesema uwezo wa kufuatilia ufanisi, mwenendo na kutoa ripoti za safari za ndege ni muhimu ili kuhakikisha usalama wa abiria na wafanyakazi, pamoja na jamii zilizoko chini.
Ugonjwa wa kipindupindu na kuharisha umeongezeka mara dufu nchini Yemen mbali na zahma nyingine kama njaa, ukosefu wa mahitaji muhimu na mahangaiko ya vita kila uchao.