Dungusi kakati ni jibu la njaa- FAO
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema majani na matunda ya dungusi kakati ni suluhu ya ukosefu wa chakula kwa binadamu na mifugo katika maeneo yenye ukame.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema majani na matunda ya dungusi kakati ni suluhu ya ukosefu wa chakula kwa binadamu na mifugo katika maeneo yenye ukame.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti ya utekelezaji wa azimio lake la ambalo pamoja na mambo mengine linalaani uharibifu na usafirishaji wa mali za kitamaduni kwenye eneo yenye vita, kitendo ambacho kinafanywa na vikundi vya kigaidi.
Lengo namba 4 la malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, linapigia chepuo elimu bora. Hii inamaanisha pamoja na mambo mengine watoto siyo tu waandikishwe shule bali pia wamalize masomo yao hadi mwisho bila kukosa.
Tamasha la kimataifa la ushirika wa Kusini-Kusini mwaka 2017 leo limekunja jamvi mjini Antalya Uturuki huku umoja wa Mataifa na wadau wakifurahia matokeo .
Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwe lile la mpango wa chakula duniani WFP na lile idadi ya watu ulimwenguni UNFPA yameazimia kushirikiana hii leo katika suala la kuwekeza katika maendeleo ya vijana barubaru wa kike nchini Laos.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji duniani, ni lazima yajumuishe watoto waliolazimika kuondoka makwao kutokana na sababu mbalimbali.
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na wapalestina, ili kujadili mustakabali wa eneo hilo ambalo limekuwa katika migogoro kwa miongo zaidi ya mitano.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu harakati za kutokomeza silaha za nyuklia huku hoja ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora la masafa marefu usiku wa kuamkia leo ikipatiwa kipaumbele.
Katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs au ajenda 2030, vijana kama nguvu kazi na mustakabali wa dunia wanapewa jukumu la kijiendeleza ili kujikwamua na suala la umasikini siku za usoni.
Shirikia la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limekaribisha uamuzi wa Libya wa kuanzisha kituo cha mpito kwa ajili ya wahamiaji huko Tripoli ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuimarisha ulinzi wa kundi hilo.