Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 MACHI 2024

27 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia, na mchango wa wasanii katika msaada wa kibinandamu nchini DRC. Makala tunamulika mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji na mashinani tunasalia nchini DRC, kulikoni?

  1. Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo.
  2. Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. 
  3. Makala tunaangazia mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji umesababisha mamia kwa maelfu ya familia kuwa wakimbizi, ambao wanaendelea kutatizika kutafuta chakula, malazi na usalama.
  4. Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe wa mlinda amani wa kuhusu elimu kwa wasichana.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'8"