Ujenzi wa kuhimili tabianchi warejesha furaha kwa watoto na wazazi Msumbiji
Baada ya kimbunga Idai kupiga Msumbiji mwezi Machi mwaka 2019, maisha ya watoto ‘yalitumbukia nyongo’ kwani hawakuwa ten ana matumaini ya mustakabali wao, halikadhalika wazazi wao. Mapaa ya shule yalienguliwa, hospitali zilitwama, halikadhalika makazi yao.