Inspekta mkuu Doreen Malambo ambaye ni mshauri wa masuala ya kijinsia kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) ameshinda tuzo ya mwaka ya Umoja wa Mataifa ya afisa wa pilisi kwamwaka huu 2020 kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kusaidia vikundi vilivyo hatarini kama wanawake, wasichana , Watoto na watu wenye ulemavu.
Kutana na Kayumba Chiwele mwanaharakati wa masuala ya afya ya akili nchini Zambia na pia mshindi wa tuzo ya Benki ya Dunia ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs katika kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika iliyotolewa mwishoni mwa wiki.
Kutana na Kayumba Chiwele mwanaharakati wa masuala ya afya ya akili nchini Zambia na pia mshindi wa tuzo ya Benki ya Dunia ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs katika kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika iliyotolewa mwishoni mwa wiki. Yeye na shirika alilolianzisha la PsychHealth wanapigia upatu upatikanaji wa huduma za afya ya akili hasa wakati huu wa janga la corona au CIVID-19.
Zambia ni moja ya nchi tisa kusini mwa Afrika ambazo zinakumbwa na janga au viwango vya dharura ya ukosefu mkubwa wa uhakika wa chakula. Familia zinakabiliwa na hali mbaya kutokana na hali mbaya ya hewa kusababisha mavuno kuwa mabaya mwaka hadi mwaka na ni dhahiri hali ingekuwa mbaya zaidi kama si msaada kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau, ambao unaleta mabadiliko makubwa katika katika maisha ya kila siku ya watoto na familia zao.
Nchini Zambia, mradi wa maji uliofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, umekuwa nuru kwa wakazi 800,000 wa wilaya ya Gwembe kusini mwa Zambia