Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2024 tishio kwa watoto: Ripoti ya UNICEF

Mvulana akitembea kwenye vifusi vya nyumba zilizoharibiwa katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
© UNICEF/Eyad El Baba
Mvulana akitembea kwenye vifusi vya nyumba zilizoharibiwa katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Mwaka 2024 tishio kwa watoto: Ripoti ya UNICEF

Afya

Duniani kote mwaka 2024, watoto wanatarajiwa kuona kuongezeka kwa matukio ya ghasia, vita na matatizo ya kiuchumi, linasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), katika utafiti uliotolewa siku ya Jumatatu ya Januari 15, 2024.

Kila mwanzo wa mwaka, UNICEF huchunguza hatari ambazo watoto wanaweza kukumbana/ kukabiliana nazo, na kupendekeza njia za kupunguza madhara yanayoweza kutokea.

Ripoti ya hivi karibuni iliyopewa jina la Matarajio ya Watoto 2024: Ushirikiano katika Ulimwengu uliogawanyika, inatoa taswira ya mustakabali wa siku zijazo za muda mfupi kuendelea kwa migogoro na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi.

Maelezo na mwelekeo muhimu wa kuzingatia

Vurugu na vita inayoendelea

Matarajio ya migogoro, inasema ripoti hiyo, yatachochewa na kuongezeka kwa ushindani kati ya mataifa yenye nguvu duniani, na kutishia haki na maisha ya watoto, mbali na madhara ya mara moja kwa maisha ya watoto, vurugu na vita huathiri watoto kwa kuelekeza rasilimali kutoka kwenye elimu, huduma za afya na lishe.

Zaidi ya watu 5,000, ikiwa ni pamoja na watoto 3,500, walipoteza nyumba zao katika moto uliotokea katika kambi ya wakimbizi nchini Bangladesh.
© UNICEF/Salim Khan
Zaidi ya watu 5,000, ikiwa ni pamoja na watoto 3,500, walipoteza nyumba zao katika moto uliotokea katika kambi ya wakimbizi nchini Bangladesh.
Kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi

Ukuaji wa uchumi usio na kasi unadhoofisha miaka ya maendeleo/ mafanikio  katika kupunguza umaskini wa watoto na kufanya kuwa vigumu kwa vijana kufikia soko la ajira duniani, ikiwa biashara ya kimataifa itakwama kwa sababu za kutokuaminiana na kutoa kisasi kwa njia ya ushuru, bei za vyakula zinaweza kuongezeka, na lishe ya watoto inaweza kuathirika.

Njia ya kuwalinda watoto, inasema ripoti hiyo, ni mshikamano wa kiuchumi, ushirikiano wa soko, na uwekezaji katika stadi za siku zijazo.

Ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa

Ripoti inaeleza wasiwasi wake kwamba mfumo uliogawanyika wa kimataifa hautoi maswala muhimu kwa Watoto, hii inaweza kupunguza juhudi za kushughulikia ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto; kuzuia juhudi za kimataifa kushughulikia hatari, ikiwa ni pamoja na janga la tabianchi; na kuzuia hatua za pamoja zinazohitajika kuzuia na kumaliza migogoro. 

Mfumo wa kimataifa una nafasi ya kurekebisha mwelekeo wake kwa mwaka 2024 kupitia hatua Madhubuti, utawala wa kimataifa, na mageuzi ya fedha.

https://twitter.com/UNICEF/status/1746955468608585989 

Ukosefu wa usawa katika nchi zinazoendelea

Nchi zinazoendelea bado zinakabiliwa na ukosefu wa usawa wa kimuundo wa kifedha, hii ina maana kwamba rasilimali, fursa, na nguvu hazigawi sawa, na hivyo kupunguza uwezo wa nchi kuwekeza kwa watoto. 

Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi wanategemea fedha kutoka nje ili kufidia gharama za afya na elimu, teknolojia mpya na na mageuzi katika utoaji mikopo yanaweza kutoa matumaini kwa mustakabali wa usawa zaidi.

Watoto wanatengeneza umbo kwa mikono yao katika wilaya ya Omo kusini mwa Ethiopia.
© UNICEF/Raphael Pouget
Watoto wanatengeneza umbo kwa mikono yao katika wilaya ya Omo kusini mwa Ethiopia.
Demokrasia chini ya tishio

Chaguzi nyingi zitafanyika mwaka wa 2024, na demokrasia ya kimataifa itakabiliwa na hatari ambazo hazijawahi kushuhudiwa, zinazotolewa na taarifa potofu na vurugu za kisiasa, zinazotishia haki na huduma za Watoto, watoto na vijana wanaweza kuathiriwa zaidi na unyanyasaji huu, ambao unaweza kusababisha kifo, madhara ya kimwili au ya kihisia, kukatizwa kwa huduma za umma na kufungwa kwa shule, vijana wanaonyesha kutoridhika na demokrasia, lakini wanaelekeza nguvu zao katika hatua za kujenga za kiraia, na uharakati wa mtandaoni.

Janga la tabianchi

Mabadiliko ya haraka kuelekea nishati endelevu unatengeneza upya madini muhimu na soko la ajira, jambo ambalo huleta manufaa makubwa kwa watoto na vijana, lakini pia huleta hatari kwa vile zina uwezekano wa kukabiliwa na, kwa mfano, utendaji hatari wa kazi katika jumuiya za wachimbaji madini.

Mpito wa kijani pia hubadilisha matarajio yao ya ajira katika uchumi unaozingatia mazingira, na unaweka changamoto kwa serikali kushughulikia mahitaji katika elimu na mafunzo ya ujuzi, lakini, ikisimamiwa kwa uwajibikaji, ushirikiano na kwa haki, mpito huu unaweza kuwa chanya kwa watoto.

Watoto wanacheza kwenye ardhi kavu iliyokauka kusini mwa Pakistan.
© UNICEF/Vlad Sokhin
Watoto wanacheza kwenye ardhi kavu iliyokauka kusini mwa Pakistan.

El Niño, magonjwa yanayoenezwa na mbu na upungufu wa maji pia vitatishia afya na ustawi wa watoto, na kusababisha ukosefu wa chakula, ongezeko la hatari ya watoto na uhamishwaji wa nguvu, ushirikiano mkubwa wa kimataifa katika usimamizi wa hatari za mazingira na uvumbuzi wa teknolojia unaweza unaweza kupunguza athari hasi.

Udhibiti wa Akili Mnemba (AI)

Hatimaye, athari za ukuaji usiokubalika wa teknolojia ikiwa ni pamoja na AI, zinachochea hofu na wasiwasi kuhusu ustawi wa Watoto, sera ya udhibiti unaokuja ikiwa itazingatia mahitaji ya watoto na kubuniwa kwa uwajibikaji, unaweza kutoa fursa na kupunguza athari hasi.

Wakati wa kufanya uamuzi

Hitimisho lililofikiwa na mwandishi wa ripoti hii ni kwamba dunia inakabiliwa na chaguo kati ya mustakabali wa kugawanyika na kutofautiana zaidi au ule wa ushirikiano na kushirikiana, ambapo fursa zinatumika kujenga dunia yenye usalama na usawa zaidi kwa watoto.