Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

AI

Utafiti wa Shirika la Kimataifa la Kazi umebaini kuwa kazi nyingi na viwanda vitakunufaika na Akili Mnemba lakini ajira kama za ukarani zitachukuliwa na Akili Mnemba kwa kiasi kikubwa.
© Unsplash/Steve Johnson

UNESCO yawaleta pamoja wadau wa AI na Filamu kujadili fursa na changamoto zinazowakabili

Akili mnemba (AI) imebadili fani ya sanaa na utamaduni kwa njia ambazo haikutarajiwa. Hata hivyo mabadiliko hayo ni ya muda mrefu. Ili kuwapa Jukwaa wataalam wa Sanaa na dijitali, shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mkutano maalum ili kujadili athari za akili mnemba kwenye sekta ya filamu.

07 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Magavana Dkt. Wilber Ottichilo wa Kaunti ya Vihiga na Gavana wa Kaunti ya Narok, Patrick Ole Ntutu hivi karibuni walipohudhuria Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu SDGs lijulikanalo kama HLPF hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, waliketi na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ili waeleze mipango yao ya kutimiza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika majimbo yao huko nchini Kenya.

Sauti
9'58"